WAZIRI
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) ameishutumu Mamlaka ya
Mapato (TRA) kuwa ni kikwazo kwake katika utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya kuboresha bandari ya Dar es Salaam ikiwa nipamoja na
utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).
Dk.
Mwakyembe alisema watu wengi wanaoitumia bandari ya Dar es Salaam (TPA)
wanalalamikia madudu wanayofanya TRA hasa tatizo la kufeli kwa mfumo
wa mawasiliano ya kompyuta unaotumiwa na mamlaka hiyo kutoza kodi
mbalimbali.
Alitoa
shutuma hizo baada ya kutakiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ajibu
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Watanzania wanaofanya biashara na wale
wanaoishi katika jiji la Guangzhou, jimbo la Guangdong ambalo ni jiji
kubwa la biashara lililoko kusini mwa China.
Jana usiku (Alhamisi, Oktoba 24, 2013)Waziri
Mkuu alihitimisha ziara yake ya China kwa kufanya mazungumzo na
Watanzania wanaoishi katika jimbo hilo maarufu kwa biashara.
Bw.
Stanley Mwakipesile ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo anayefuata
bidhaa zake katika jimbo la Guangzhou, katika hoja zake alisema utoaji
wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ni tatizo kubwa kutokana na
mfumo wa kutoza kodi unaotumiwa na TRA kutofanya kazi siku zingine na
hivyo kusababisha mteja kutozwa fedha nyingi.
Mfanyabiasahra
huyo alisema kutokana na kero hiyo, wafanyabiashara wengi kutoka nchi
jirani wameikimbia bandari hiyo na sasa wanatumia bandari ya Mombasa
jambo ambalo alisema ni hasara kwa nchi. “Inakuwaje
kila siku pale TRA system inakuwa down? Kuna urasimu mwingi tu pale
lakini cha ajabu wakati wao ndio hawafanyi kazi, lakini mteja anatozwa
eti kachelewesha kutoa mzigo,” alisema Mwakipesile.
Dk.
Mwakyembe katika kujibu hoja za mfanyabiashara huyo alikiri kuwepo kwa
tatizo hilo na akasema eneo linalolalamikiwa sana ni TRA ni kuwatoza
wateja tozo za ziada hata kipindi ambacho watendaji wa mamlaka hiyo
hawafanyi kazi kwa kisingizio cha mfumo kutofanya kazi (system down).
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwa kweli TRA ni tatizo, hasa hili la system down kwa
kweli ni kero na linawaumiza watu wengi wanaotumia bandari yetu. Ni
lazima tukae tuone namna ya kutatua tatizo hili,” alisema Mwakyembe.
Alisema
licha ya kuwepo agizo kutoka serikalini la kutaka TPA na TRA wafanye
kazi saa 24, lakini watendaji wa TRA wanafanya kazi kwa saa 12 tu na
wanalala kwa siku 10 katika mwezi mzima.
Alisema
wakati TRA wanaenda kulala, mteja hahudumiwi na wanapokuja kuendelea
na kazi kesho yake, wanawatoza wateja tozo ya kuchelewesha mzigo
wakati makosa siyo ya wateja bali ni ya watendaji wa mamlaka hiyo ya
kukusanya kodi kwa Tanzania.
“Sisi
TPA hatulali; lakini wenzetu hawa wanalala, inakuwaje wanaenda kulala
wakati mizigo imerundikana pale bandarini? Kwa kweli hawa watu ni lazima
tushughulike nao.
“Mimi
nimesaini BRN, Rais anataka kuona mwaka 2015 shehena inaongezeka pale,
na kufikia tani 18 sasa yule atakayekaa mbele yangu kunikwamisha mie
nitampitia,” alisema Dk Mwakyembe na kushangiliwa kwa nguvu na
watanzania hao.
Hata
hivyo aliwatoa hofu Watanzania kwa bandari ya Dar es Salaam inafanya
kazi vizuri na kila mwaka shehena imekuwa inaongezeka, hali inayoonyesha
kuwa batu nchi nyingi ikiwemo Zimbabwe bado zinatumia bandari hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, OKTOBA 25, 2013
No comments:
Post a Comment