Shirika
la Mpango wa Chakula wa Umoja la Mataifa (WFP) linaadhimisha Siku ya
Chakula Duniani tarehe 16 Oktoba kwa kusisitiza umuhimu wa lishe katika
kumbadilisha mtu mmoja mmoja, jamii na uchumi wa taifa, na umuhimu wa
kuifanya lishe kama suala la msingi katika mipango yote ya maendeleo.
“Wasichana
na wavulana wenye lishe duni wanapata changamoto za kiafya , hawawezi
kufanya vizuri shuleni, na baadaye inakuwa vigumu kwao kufanya vizuri
katika sehemu za kazi, na hii inadumaza uwezo wao wa kibinadamu na uwezo
wa kuchangia kwenye jamii wanamoishi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa
WFP Ertharin Cousin.
“Kwa
kutoa kipaumbele katika lishe leo tunawekeza kwa ajili ya mustakabali
wetu wa jumla wa kimataifa wa baadaye. Uwekezaji ni lazima uhusishe
chakula, kilimo, afya na mifumo ya elimu,” alisema.
Leo
hii takribani watu milioni 842 - yaani zaidi ya mtu mmoja katika kila
watu nane duniani - wanakabiliwa na njaa iliyokithiri. Zaidi ya hayo -
takriban watu bilioni mbili – wanakosa vitamini na madini yanayohitajika
kwa afya.
Kama
jumuiya ya kimataifa ingewekeza dola bilioni 1.2 kwa mwaka kwa miaka
mitano katika kupunguza upungufu wa viiini lishe, matunda yake yake
katika afya bora, kupungua vifo vya watoto na kuongezeka kwa kipato,
yangeleta faida ya dola bilioni 15.3.
Ukurasa
wa 2 “Hapa Tanzania, kutatua tatizo la lishe duni ni sehemu muhimu ya
shughuli za mpango wetu na shughuli zetu za kisera,” alisema Mkurugenzi
Mkazi wa WFP Tanzania Richard Ragan.
“Tunawafikia
watu milioni 1.2 walio kwenye hali tete kila mwaka, na kupitia mipango
yetu ya lishe tunahakikisha akina mama, wajawazito, na watoto wanapata
chakula bora na chenye lishe.
Kauli
mbiu ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu ni “Mifumo Endelevu ya
Chakula kwa Usalama wa Chakula na Lishe.” WFP inatoa msaada wa chakula
kwa watu milioni 97 duniani kote. Hapa ni baadhi ya njia ambazo WFP
inalenga kwenye lishe:
• Kuongeza idadi ya watoto na akina mama ambao wanapata vyakula vilivyoongezewa virutubishi;
•
Kutilia mkazo lishe katika siku 1000 za muhimu – tangu ujauzito mpaka
mtoto anapofikisha miaka miwili - ambapo mtoto anahitaji sana lishe kwa
ukuaji mzuri;
•
Kuongeza msaada kwa kutoa fedha taslimu na/au vocha kipindi ambapo
chakula kinapatikana kwenye masoko, ili watumiaji waweze kununua vyakula
vya aina mbalimbali vinavyopatikana kwenye maeneo yao;
• Kusisitiza ulaji wa vyakula anuai kutoka katika makundi muhimu kwenye mipango ya mlo shuleni, kwa kushirikiana na jamii;
•
Kushirikiana na wadau binafsi na taasisi za utafiti kutathmini faida
zinazotokana na mchele ulioongezewa virutubishi kwenye mlo wa shule;
•
Kusaidia kujenga hoja kupitia tafiti ambazo zitaongoza nchi mbalimbali
kwenye sera na mikakati ya lishe, kama vile ile ya karibuni
inayojulikana kama “Utafiti wa Gharama ya Njaa Afrika” (Cost of Hunger
in Africa survey).
“Nchini
Tanzania, WFP inafanya kazi na serikali kusukuma mbele ajenda ya lishe.
Mwezi Mei mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilizindua mpango wa kitaifa
wa kuongeza virutubishi kwenye vyakula vikuu ambavyo ni unga wa ngano,
mafuta ya kupikia, na unga wa mahindi,” alisema Richard Ragan. “Kufuatia
ukweli kwamba vyakula hivi vitazifikia kaya nyingi nchini kote, WFP
inajisikia fahari kubwa kutoa msaada wa kitaalamu kuhakikisha
wasagishaji wakati na wadogo wako tayari kuanza zoezi la kuboresha
vyakula hivi mwaka ujao.”
WFP
inasherehekea Siku ya Chakula Duniani pamoja na mashirika dada ya
chakula ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)
na Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
No comments:
Post a Comment