Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimpongeza
mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi kwa ahadi ya
kuichangia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama Jumla ya Shilingi milioni
mia mbili kila mwaka kwa miaka mitano,wakati mahafali ya kwanza ya
shule hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Nyamisati,wilaya ya Rufiji
Mkoa wa Pwani Mishoni mwa Wiki.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule ya WAMA NakayMA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Dkt.Ramadhani Dau akimkabidhi tuzo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa
mchango wake wa kuimarisha elimu nchini wakati wa mhafali ya kwanza ya
Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyofanyika huko.Nyamisati, Wilaya
ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mwishoni mwa wiki.Kuliua ni Mwenyekiti wa WAMA
Mama Salma Kikwete. Picha naFredy Maro
************************************************************
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS Jakaya
Kikwete ameitaka jamii kuwa na tabia ya kuwafadhili watoto yatima
na wanaoishi katika mazingira magumu katika kuwapatia elimu, chakula
na malazi ili waweze kuendesha maisha yao kwa kujiajiri au kujariwa
kwani kwa kufanya hivyo nguvu kazi ya taifa haitaweza kupotea.
Kauli
hiyo ilitolewa jana (juzi) na Rais Kikwete wakati wa
mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Wama
Nakayama iliyoko Nyamisati , wilayani Rufiji , mkoani Pwani
yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Shule
hiyo inayoendeshwa na Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA) ,ambapo Mwenyekiti wa taasisi hiyo ni Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais
Kikwete aliwashukuru watu mbalimbali walichangia shule hiyo kwa moyo
wao wa upendo na huruma ili watoto wa kike yatima na wanaoishi katika
mazingira magumu waweze kupata elimu, huku akisema kama wasi
wafadhili hao isingekuwa rahisi watoto hao kuwezeshwa kusoma shuleni
hapo.
“
Mtapata fadhila kwa Mwenyezi Mungu kwa kila mtoto atakayesoma
hapa…Mkopesheni Mwenyezi Mungu atawapa fadhila zake,”alisema Rais
Kikwete.
Kauli
hiyo pia iliungwa na mkono na Mama Salma Kikwete ambaye alisema bila
juhudi za pamoja kati ya Serikali, jamii na sekta binafsi
watoto wengi wa kundi hilo watakosa elimu.
Mama
Kikwete alisema nchi ina Watanzania milioni 44.9 kama wapo wenye uwezo
wapatao milioni tano kila mmoja akimchukua mtoto mmoja.
“
Tanzania isiyokuwa na watoto wasio matumaini inawezekana,”alisema
Mama Kikwete huku akisema kwa kufanya hivyo kuwasaidia kujikwamua
katika hali ya umasikini.
Rais Kikwete aliwataka
wanafunzi hao kuwa na malengo ya kupata elimu ya juu ili waweze
kukabiliana na changamoto mbalimbali na kulisaidia taifa, huku
akisisitiza wawe jasiri kusoma fani ambazo wanawake wengi wanaogopa
kuzisoma ambazo zitawawezesha kuwa mabingwa mafano udaktari, wahandisi
na wanasheria.
“
Hamna budi kushukuru na kujipongeza ombi langu ni kuweni watoto wema
heshima na mabalozi wa shule hii. Shule hii itakapokamilika huduma
zitakuwa bora.Shule hii ina kila sababu ya kuwa shule bora,” alisema
Rais Kikwete.
Aidha Rais
Kikwete alizitaka halmashauri nchini kuendelea kushishirikiana na
Maendeleo(WAMA) kuwatambua watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira magumu ili waweze kupata elimu kwa malengo
ya taasisi hiyo.
Katika
mahafali hayo Mwenyekiti wa kammpuni za IPP, Reginald Mengi aliahidi
kuchangia shule hiyo Sh. milioni 200 kwa kila mwaka kwa kipindi cha
miaka mitano na Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama cha Mapinduzi
(UWT)uliahidi kutoa Sh. milioni 10 yakiwemo mashirika mbalimbali
yaliyoahidi kutoa michango kadhaa.
Rais Kikwete
katika mahafali hayo aliwatunuku vyeti wanafunzi 67 na kutoa zawadi za
vyeti na fedha tasilimu kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri,
ambapo mwanafunzi aliibuka mshindi baada ya kufanya vema kwenye masomo
ya biashara, historia na Kiingereza.Mwanafunzi aliyefanya vizuri kila
somo alipata Sh. 100,000 na mwalimu Sh. 500,000.
No comments:
Post a Comment