MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi
Simba na Yanga iliyochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000.
Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo namba 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh.
15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Ni tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za
VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi
hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh.
37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 14,596,253.39.
No comments:
Post a Comment