Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume.
Hii
inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa
mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado
nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi
kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi wa kina
kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.
Zifuatazo
hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye
anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:
1. KUCHELEWA: Kuna
wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala
ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara
tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali
soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi
ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.
2. KUBADILI MAENEO: Hebu
chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu,
hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba
fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma
na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu
mwenendo mbaya.
Siyo
lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama
kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi,
mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.
3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa
yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa
katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na
fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali
kama nyumba kwa siri.
4. KUANZISHA VURUGU: Kuna
wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na
mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya
amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.
Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.
5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke
anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani
hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa
wanashiriki.
Husita
kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita
kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.
6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke
anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni
kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza
kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya
ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.
7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima
atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake.
Anaweza
kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri
itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara
nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa
katika hatua zake za awali za kutoka nje.
8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati
mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume
anaona vipi , wanaweza kuachana.
Kama
kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni
kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke
anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe
No comments:
Post a Comment