Sunday, October 13, 2013

TEA kuwaongeza uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi.


 Afisa Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar Es Salaam juu ya ufadhili wa Mamlaka hiyo kwa  kushirikiana na kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) kwa mafunzo ya kuongeza uwezo wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) Martha Saivoiye.
 Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe  akielezea mipango ya Mamlaka hiyo ya kuendelea kutafuta wafadhili zaidi ili kuongeza idadi ya wanafunzi  kike wanaosoma  masomo ya Sayansi,katikati ni Afisa Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda na kushoto ni Meneja Mawsiliano na Misaada kwa Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) Martha Saivoiye.
 Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) Martha Saivoiye akielezea  mikakati ya Kampuni hiyo kuongeza ufadhili  ili kuwa na idadi ya wanafunzi  wa kike wanaosoma  masomo ya Sayansi, katikati ni Afisa Mwandamizi toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Masozi Nyirenda na kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe 

 Mratibu wa kozi ya awali toka Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam(DIT)  Mhadhiri Matara Ryoba akielezea namna ya kupata wanafunzi na uendeshaji wa kozi, kulia Afisa Habari toka Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.

No comments:

Post a Comment