Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Timbulo
‘Timbulo’, amewaomba mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini, wajiandae
kupokea kibao chake kipya kinachokuja kwa jina la ‘Bado Inatamba’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Timbulo alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho,
ambacho anaamini kitakuwa gumzo mtaani kutokana na ujumbe uliopo.
Alisema wimbo huo utakuwa ni changamoto kwa wasanii
wenzake, kutokana na baadhi ya ujumbe uliopo ndani ya wimbo huo unaowaonya
wasanii kuwa na nyimbo zenye manufaa kwa jamii.
“Kiukweli wasanii wengi wa bongo fleva, tumekuwa
tukipeleka mawazo yetu kwenye mapenzi pekee, mimi nimeona kuondoka kwenye
mapenzi na kufanya kazi ambazo zinaelimisha jamii kwa kiasi kikubwa,” alisema
Timbulo.
Licha ya kutaka
kutoka na kibao hicho, Timbulo alishawahi kutamba na vibao vyake kama, ‘Samson
na Delila’, ‘Timbulo wa leo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri katika muziki wa kizazi kipya
No comments:
Post a Comment