Thursday, October 24, 2013

Watalii mbalimbali ndani na nje ya nchi watakiwa kutangaza utalii



Washindi wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na Mwenzake Mark wakitembezwa na kuangalia namna walemavu wa kituo cha Shanga River House cha jijini Arusha, washindi hao waliopatikana kupitia kampuni ya  My Destination walikuwa nchini na kutembelea vivituo mbalimbali vya utalii na kukagua miradi mbalimbali kama hiyo.
Mshindi wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling  akipuliza kioo kilicho yeyushwa  tayari kwa kutengenezwa chombo chochote ambavyo hutokana na taka ngumu zinazozalishwa na binadamu ikiwa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha shanga river house cha jijini Arusha.
 Allex na Mark wakipewa maelezo ya shughuli za kituo.

WADAU mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuutangaza utalii wa Tanzania katika maeneo yao ili kuwavutia watalii wengine kuzidi kufika kwa wingi hapa nchini kujionea maliasili zilizopo na kuchangia pato  la taifa kwa ujumla.

walipewa zawadi na marafiki mbalimbali.


Hayo yalielezwa jana na Afisa Mtendaji  wa TATO ,Sirili Akko wakati akizungumza na wadau wa maswala ya utalii waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza vijana wawili walioshinda shindano lililoandaliwa na  kampuni ya My Destination lililoshirikisha washiriki  122 ulimwenguni.

Aidha alisema kuwa ,Tanzania ni nchi ambayo imebahatika kupata vivutio mbalimbali vya utalii hivyo kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili zetu, hivyo hawana budi kuutangaza utalii wetu katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa nchi za Afrika.


Alisema kuwa, shindano hilo lilihusu mshiriki kuchagua vitu ambavyo wangependa kufanya maishani kabla hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki katika shindano hilo na kuoanisha kuwa wao wangependa kutembea dunia nzima na kujionea maajabu yaliyopo katika vituo mbalimbali.

‘baada ya vijana hao kushiriki shindano hilo walishinda na kupewa nafasi ya kuchagua  kutembelea nchi 25 kati ya 80 ambazo katika hizo nchi 25 walichagua nchi tatu za Afrika ikiwemo kutembelea Tanzania,Zimbabwe,na Afrika ya kusini na ndo maana wapo hapa leo tayari kwa kuanza zoezi hilo’alisema Akko.

Aliongeza kuwa, kitendo cha wao kuchagua Tanzania kati  ya nchi 25 kimewafariji sana wao kama wadau wa utalii kwani imeonyesha jinsi ambavyo utalii wa nchi yetu unaweza kutangazwa na watalii mbalimbali na hatimaye kuweza kupata wageni wengi zaidi kwa kujionea maliasili zilizopo katika maeneo yetu.

Nao vijana hao walioshinda shindano hilo kutoka Calfonia Alex Ayling na Mark Ayling  walisema kuwa, shindano hilo waliweza kushinda  baada ya kukithi viwangovya shindano hilo na hatimaye wamefurahia sana kushinda kwani mchuano uliwashirikisha watu mbalimbali ulimwenguni.


Alex alisema kuwa, lengo la kuchagua Tanzania miongoni mwa nchi tatu za Afrika ambazo wangependa kutembelea ni kutokana na uoto wa asili uliopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao

Alisema kuwa,katika maeneo hayo yote watakayotembelea watakuwa wakichukua mikanda mbalimbali kwa ajili ya kuirusha kwenye mtandao na hatimaye watu mbalimbali kuweza kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika  vituo watakavyotembelea.

Mark alisema kuwa, wamekuwa wakifuatilia vitu  mbalimbali vinavyoendelea Tanzania ikiwemo wanyama mbalimbali wa kuvutia , pamoja na kufuatilia makabila ya wamasai ambayo watakuwa na nafasi ya kuwatembelea na kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao.

No comments:

Post a Comment