Na Edwin Moshi, Makete
Baada ya zoezi la bomoa bomoa kwa hiari ndani ya mwezi mmoja
kumalizika eneo la Makete mjini wilayani Makete, hii leo zoezi hilo
limetekelezwa kwa nguvu ya serikali kwa wale ambao hawakubomoa ama
kumalizia kubomoa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara ya lami
Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa kwa hiari lilimalizika Oktoba 09
mwaka huu, ambapo kwa kiasi kikubwa mtandao huu ulishuhudia wananchi
wakibomoa nyumba zao wenyewe huku wengine wakitekeleza nusu
Mtandao huu umeshuhudia katapila likiendelea na shughuli ya
kupakia masalia ya majengo yaliyobomolewa, huku likibomoa baadhi ya
majengo ambayo yalikuwa hayajabomolewa pamoja na yale yaliyobomolewa
nusu
Baadhi ya watu walionekana wakiendelea na kubomoa nyumba zao huku
wengine wakiokoa baadhi ya vitu ambavyo walidhani vingewafaa kwa
shughuli za ujenzi kwenye maeneo mengine
Hii inaashiria ujenzi huo wa barabara kwa kiwango cha lami eneo la Makete mjini unaanza kwa kasi kama inavyotarajiwa na wengi
No comments:
Post a Comment