Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo
kwenye Ukumbu wa Idara ya Habari-Maelezo,wakati wa kutangaza udhamini wa
Mbio ya Uhuru Marathon.Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya
Mbio za Uhuru Marathon Tanzania,Innocent Melleck
Katibu
wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za Uhuru Marathon Tanzania,Innocent
Melleck (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es
Salaam leo juu ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
kinywaji chake kisicho na kilevi cha GrandMalt ambapo kimetoa jumla ya
shilingi milioni ishirini (20,000,000).kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah.
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha
GrandMalt imejitokeza kudhamini mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kwa
kiasi cha Sh milioni 20.
Akitangaza
udhamini huo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa TBL, Fimbo
Butallah alisema, wameona ni vyema kudhamini mbio hizo kwani zina lengo
zuri zaidi la kuimarisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa
Watanzania.
Naye
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck aliwaomba
Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo zina nia
kubwa ya kutukumbukusha wajibu wetu wa kutunza na kulinda amani, umoja
na mshikamano miongoni mwetu.
Mbio
hizi zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam hapo Desemba 8, mwaka
huu ambapo zitaanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders club.
Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kushiriki mbio hizi, huku wabunge zaidi ya
100 wakiongozwa na Spika Anne Makinda wakiwa wamejisajili kwa ajili ya
kushiriki.
Mbio
hizo zimegawanywa katika makundi makuu manne ambayo ni kilomita 3 kwa
ajili ya viongozi, kilomita 5 kwa watu wote na kilomita 21 na 42 ambazo
ni maalum kwa wakimbiaji nguli.
No comments:
Post a Comment