Monday, November 4, 2013

Inatisha! Hivi ndivyo alivyojeruhiwa Dk Mvungi


Mtoto wa Dk. Sengodo Mvungi, Deogratius Mwarabu (kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku (katikati), na Prof. Paragamba Kabudi walipofika MOI kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye amefikishwa MOI baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga. 



 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengodo Mvungi akitolewa katika chumba cha huduma za dharura MOI na kupelekwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa. 

Dk. Sengodo Mvungi akipata matibabu ndani ya gari la kubeba wagonjwa wakati akipelekwa hospitali ya Aga Khan.



Dk. Sengodo Mvungi akiwa na majeraha kichwani na sehemu za paji la uso.
Na Hapiness Katabazi

MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.

Dk. Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.

HABARI MSETO

No comments:

Post a Comment