Mabingwa wa mbio za
mitumbwi zinazodhaminiwa na bia ya Extra Lager ,kikundi cha nahodha
Mhete Muhoja wakiwasili katika ufukwe wa Monarch wakati wa mbio hizo
zilizofanyika mwishoni mwa wiki.
Washiriki wa mbio za
mitumbwi zinazodhaminiwa na bia ya Balimi Extra Lager wanawake Ukerewe
wakianza rasmi mbio hizo zilizofanyika katika Ufukwe wa Monarch Ukerewe
mwishoni mwa wiki.
KIKUNDI cha
Nahodha Totoji Mazinge Ngoroma kutoka Wilayani Ukerewe kimetwaa ubingwa wa
mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini kupitia
Bia ya Balimi Extra Lager na hivyo kujitwalia zawadi ya fedha taslimu Shilingi
900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika mashindano
ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Toto Sebastiani ambao walizawadiwa
fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Kisiwa cha
Ukerewe pia katika fainali za Kanda pale jijini Mwanza ,nafasi ya tatu
ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Simon Fundi ambao walizwadiwa fedha taslimu
shilingi 500,000
Upande wa
Wanawake kikundi cha nahodha mwanamama Mhete Muhoja nakujitwalia ubingwa na
hivyo kuzawadaiwa fedha taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe kwenye mashindano ya Kanda pale jijini Mwanza
mwezi ujao.
Nafasi ya
pili upande wa wanawake ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Jenifer Elias na
ambao walijinyakuliwa zawadi ya fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na
kuwakilisha kisiwa kwenye fainali za Kanda upande wa Wanawake pale jijini
Mwanza,nafasil ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Edna Chambo ambao
walizawadiwa fedha taslimu shilingi 400,000.
Akizungumza
na wananchi waliofurika kwa wingi katika ufukwe wa Monarch Galu Beach meneja
mauzo wa TBL wilaya ya Ukerewe, Josephat Changwe amesema kuwa licha ya mchezo
huo kuwa burudani Kampuni yake imenuia kuyaboresha mashindano hayo ili yapate
sura ya kimataifa huku yakibadili maisha ya wananchi kama sehemu ya mitaji.
Fainali za
Kanda za mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Decemba 7,2013, katika ufukwe
wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo watashindana mabingwa wa Kanda nzima ambao ni
kutoka Kigoma, Kagera,Ukerewe,Musoma na wenyeji Mwanza.
No comments:
Post a Comment