USAJILI wa mbio za Uhuru
Marathon, unatarajiwa kuanza kutingisha wengi wakati Spika wa Bunge, Anne
Makinda leo katika Viwanja vya Bunge, anatarajiwa kuwaongoza wabunge mbalimbali
kujisajili kwa ajii ya kushiriki mbio hizo.
Katibu wa Kamati ya Uhuru
Marathon, Innocent Melleck alisema, Makinda anatarajiwa kujisajili ili
kushawishi wabunge wengi kushiriki mbio hizo ambazo lengo lake kubwa ni
kusisitizia umoja, amani na mshikamano uliopo miongoni mwa Watanzania.
Melleck alifafanua kuwa,
fomu hizo zitatolewa kwa Sh 100,000 kwa wale watakaokimbia mbio za kilomita
tatu, Sh 2,000 mbio za kilomita tano, Sh 6,000 kwa atakayeshiriki moja kati ya
mbio za kilomita 21 au 42.
“Hizi mbio ni muhimu zaidi
kwa ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa Watanzania wote wakashiriki ili
kuipigania amani iliyopo nchini mwetu na ndiyo maana hata Rais Jakaya Kikwete,
pia atashiriki.
“Kesho (leo) Spika Makinda
anatarajiwa kuwaongoza pia wabunge wanaotaka kushiriki mbio hizo na ni imani
yetu wajitokeza kwa wingfi kushiriki,” alisema.
Mratibu huyo alisema mbio
za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali,
wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa
ajili ya watu wa mahitaji maalumu.
No comments:
Post a Comment