RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogondogo wakiwemo Katibu Mkuu wa
zamani, Fredrick Mwakalebela na Makamu wa pili wa TFF aliyemaliza muda wake,
Ramadhani Nassib (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na
uchaguzi zitaundwa baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba
ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.
Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji
aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine
wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati
wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa
Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu
Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao
Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati
wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama,
Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said
George na Nassoro Idrissa.
Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati
wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo,
Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian
Maro.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na
Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi,
Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na
Ibrahim Masoud.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa
Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande,
Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia
Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama,
Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala,
Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra
Mohamed.
Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri
January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa,
Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na
Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein
Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan
Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza,
Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na
Elias Mwanjala.
Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.
No comments:
Post a Comment