Friday, November 29, 2013

MATEMBEZI YA DAR MPAKA MORO YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM KUANZA JANUARI 11-2014


 Ni changamoto inayotolewa mbele ya Watanzania,kukumbuka maana halisi ya  uzalendo kujitoa mhanga kuweza kufanikisha maendeleo yao wenyewe kwa kujishughulisha na kujibidisha katika nyanja mbalimbali kwa manufaa ya Taifa,kujitolea kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa,kuacha kulalama tu kuwa serikali haijawafanyia moja ama mbili lakini wao wenyewe kutambua mchango wao kama Watanzania na wajibu wao kama wananchi, kubwa zaidi kujivunia nchi iitwayo Tanzania kwa yale mema na adimu yaliyopo na kurekebisha palipo na kasoro kwa moyo mmoja bila kujali itikadi,imani, asili ama mtizamo miongoni mwetu, Tanzania,kwa nini Dar es Salaam mpaka Morogoro.Dar es Salaam imeendelea kuwa kituo kikuu cha shughuli nyingi za kiuchumi,kiserikali na vilevile ni mkoa ulio na watu wengi zaidi Tanzania, takribani milioni mbili na nusu (2.5mil) kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002, wakati Morogoro ina watu wasiofika laki tatu , na kwa ukuaji wa asilimia 4.39 kwa mwaka inaweza pia kuwa ya tatu barani Afrika na tisa duniani, hii inawakilisha tofauti kubwa sio tu kwa idadi lakini ya ukuaji, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, ukuaji wa kiuchumi na vilivile hali ya kipato na fursa za kiuchumi” alisema Chuma.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM)

No comments:

Post a Comment