Na
Mwandishi Wetu
MPANGO wa Taifa wa Damu S
alama Tanzania (NBTS) umevuka
malengo ya ukusanyaji damu kwa asilimia 110 katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi
Septemba 2013 ambapo jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka malengo ya
chupa 35,000 zilizokuwa zikusanywe.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa Mpango wa Damu Salama
Tanzania Bw. Rajab Mwenda alisema Kanda iliyongoza kwa makusanyo ya damu
ni Kanda ya Mashariki inayojumuisha
mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Dodoma na Pwani
ambako jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa, Kanda inayofuatia kwa ukusanyaji
damu ni Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro,Arusha, Manyara, Tanga) iliyokusanya chupa 6,159.
Alisema katika kipindi cha mwezi oktoba 2012 hadi
Septemba 2013 takwimu zinaonyesha chupa za damu 139,676 ambayo ni sawa na
asilimia 99.8 ya lengo la kukusanya chupa 140,000 ilifikiwa hata hivyo Mpango
wa Taifa wa damu salama unakusanya asilimia 26 ya mahitaji ya damu kwa
mwaka. Mahitaji ya damu kwa mwaka ni
wastani wa chupa 400,000- 450,000.
Alisema
tofauti iliyoko ya upatikanaji wa damu kwenye hospitali nchini imekuwa inafidiwa na ndugu wa
wagonjwa katika kuchangia damu ili
kuokoa maisha ya mgonjwa.
Bw.
Mwenda alisema mbalimbali ambazo zinasababisha mpango kushindwa kukusanya damu
kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari kunatoakana na uelewa mdogo katika jamii kuhusu uchangiaji damu kwa
hiari kwani mfumo uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa ndiyo wanatoa.
Alisema
nyingine ni uhamasishaji usiotosheleza
toka kwa viongozi mbalimbali wa jamii, wanasiasa, viongozi wa dini, uuzwaji wa
damu usio halali hospitalini jambo ambalo linawakatisha tamaa wachangia damu wa
hiari, matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na miundombinu hafifu hususan barabara duni
wakati wa kukusanya na kusambaza damu.
Bw. Mwenda alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama una
wadau mbalimbali ambao hujitokeza kuchangia damu kwa hiari kama taasisi za
kidini, majeshi, sehemu za kazi, mikusanyiko ya watu na wanafunzi ambao huchangia
asilimia 80 ya damu hapa nchini
Alisema katika kipindi cha Novemba hadi Januari kila mwaka ni kigumu katika ukusanyaji damu kwani wadau wakuu ambao ni wanafunzi wanakuwa
likizo ya mwaka hivyo Mpango
wa Taifa wa Damu Salama umeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na
changamoto hiyo.
Alisema katika
mikakati hiyo ni kufanya kampeni ya
kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari katika
jamii na sehemu za makanisani, minadani, stendi za mabasi,
misikitini, kwenye masoko na sehemu za kazi.
Alisema wameanza kuhamasisha
kambi za jeshi, makundi ya dini na ma wasiliano yamefanyika kwa jumuiya
mbalimbali hapa nchini zichangie damu mfano jumuiya ya Khoja shia, Sabato na
Jaula.
Pia alisema watatumia vyombo
vya habari ili kuikumbusha na kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchangia
damu na visaidie kutoa elimu na kutangaza
ratiba ya ukusanyaji damu katika vituo
vidogo na vikuu.
Alitoa rai kwa Watanzania kujitokeza kuchangia
damu kwa hiari katika vituo vya damu salama kwa mtu yoyote mwenye afya mwanamke
au mwanaume na mwenye umri kuanzia miaka 18 ajitokeze kuchangie damu.
Alisema uchangiaji wa damu kwa hiari
una faida kwa mtoaji kwa vile napunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kuwepo kwa
madini chuma mengi kupita kiasi katika damu kunakodhoofisha utendaji kazi na kuchangia
damu mara kwa mara hurekebisha madini
chuma ya ziada katika mfumo wa
damu.
Alisema faida nyingine ni upimaji wa
afya pasipo gharama kwa sababu wakati
unapochangia damu mtaalamu wa tiba daktari au muuguzi atapima shinikizo la damu
yako, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vya afya bure.
No comments:
Post a Comment