Mwandishi Wetu
Nyota
wa mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza
kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya
Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
Mbali
ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la
vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya
shaba.
Katika
mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na
warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa
na wadhamini hao.
Clara
alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza
kushinda katika historia. Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi
na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika
Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika
nafasi ya kwanza nay a pili.
Muandaaji
wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja
kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani
mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
“Amefanya
vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na
kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
Alisema
kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa
Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo
vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel,
Ustream na Venevisión.
No comments:
Post a Comment