Friday, December 6, 2013

KERO YA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA YAPATIWA UFUMBUZI, NAFASI KUTANGAZWA MTANDAONI



001-2Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe,Makongoro Mahanga akitoa hotuba yake. HABARI PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM 

SERIKALI imezindua mfumo maalumu wa kielektroniki wa taarifa za soko la ajira, ambao utamuwezesha mtafuta kazi kufahamu nafasi mbalimbali za kazi zinazotangazwa ndani na nje ya nchi.

Mtandao huo ambao umeelezwa kuwa utakuwa msaada mkubwa hususani kwa vijana, utamuwezesha muomba kazi kuomba nafasi hizo moja kwa moja katika makampuni husika kulingana na vigezo vitakavyokuwa vikihitajika.

Akizundua mtandao pamoja na maonyesho ya shughuli za huduma za ajira jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema, mbali na kutangaza nafasi za ajira pia mfumo huo utawawezesha watu wenye nia ya kuwekeza hapa nchini kutambua aina ya ujuzi unaopatikana nchini na kuwarahisishia katika kuajiri.

“Hii itapunguza waajiri kuajiri wageni zaidi katika zile nafasi ambazo zina wataalumu nchini kutokana na kufahamu mapema. Pia kwa wanafunzi wqa vyuo vikuu watafahamu mapema ujuzi na taalumu wanazopaswa kusoma kwa kuwa utatoa taarifa zitakazowezesha mtu kujua mahitaji ya sasa na ya siku za usoni katika soko la ajira,” aliongeza.

Kwa upande wa waajiri mfumo huo utawawezesha kutangaza nafasi za kazi walizonazo ikiwa ni pamoja na sifa za mtafuta kazi wanayemhitaji.
“Wataweza kupata wafanyakazi wenye viwango wanavyovitaka kwa urahisi kwa kujiunga na mtandao huu,” alisema.

Alisema hatua ya mtandao huo utasaidia kupunguza ukosefu vwa ajira kwa vijana kwani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lilikuwa kwa asilimia 13.4 hivyo ni matarajio kiwango hicho kitapungua baada ya waajiri wengi kutangaza ajira kupitia mtandao huo.

Mahanga ametoa wito kwa waajiri wote nchini kutumia mfumo huo kutangaza ajira na watafuta kazi na kuutumia kupata taarifa sahihi ili kuweza kuomba nafasi hizo.
Mtandao huo ambao umezinduliwa ni www.ajiralmis.go.tz, vijana wametakiwa kuutumia kwa usahihi zaidi ili kunufaika na ajira zinazotangazwa
002-2Huu ndio mtandao uliozinduliwa.
003Wanafunzi na wahitimu wa vyuo mbalimbali wakiwa kwenye kongamano la  siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi  katika  ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam. 004Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Makongoro Mahanga, akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), Boniface Chandaruba wakati akielezea kazi wanazofanya kuhusiana na ajira kwa vija mara baada ya kutembelea banda hilo, 007Wafanyakazi wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kongamano la  siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi  katika  ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment