Ankal
akimkabidhi zawadi ya Krismasi na kadi Kamanda wa FFU Ughaibuni The
Ngoma Africa Band ya Ujeruman, Ras Ephraim Makunja, a.k.a Field Marshal
wa jamii ya Annunaki walipokutana leo katikati ya jiji la Dar es salaam
na kufanya mazungumzo ya faragha ya saa moja katika kiota cha Break
Point cha mjini. Katika mazungumzo yao waliongelea mambo mengi ikiwa ni
pamoja na kuendeleza undugu uliopo baina ya Globu ya Jamii na FFU
Ughaibuni, na kupanga tarehe ambazo The Ngoma Africa Band itakuwa huru
kuja kufanya maonesho kadhaa nchini Tanzania.
Ras Makunja anarivenji kwa kumkabidhi Ankal zawadi ya moja ta T-Shirt kibao alizomletea zikiwa na logo ya Globu ya Jamii.
Ankal akimshukuru Ras Makunja kwa zawadi hiyo mwanana
Ras
Makunja akiwa na mjomba wake akijiondoa eneo la tukio taratibu huku
kakumbatia zawadi yake ya Krismasi na kadi. Meno yote arobaini yako nje
kwani hakutegemea kupata heshima hii. Picha kwa hisani ya mpiga picha wa
The Ngoma Africa Band aliyeongozana naye katika ziara hii ya mapumziko
jijini Dar es salaam. Mara ya mwisho kufika Bongo kwa Ras Makunja
ilikuwa miaka sita iliyopita, na ameshangazwa na mabadiliko na maendeleo
makubwa aliyotaona kila mahali, kuanzia nyumbani kwake mtaa wa Aggrey
ambako mbavu za mbwa yao imeshajengwa bonge la Ghorofa, nusura apotee,
na huko kwake Segerea ambako anasema kuna lami mpaka jikoni....
No comments:
Post a Comment