pacquiao na familia yake |
MARA baada
ya Desemba mwaka jana kupoteza pambano lake dhidi ya mbabe Juan Manuel Marquez kwa
‘KO’ mbabe na mbunge Manny Pacquiao alionekana kama zama za utawala wake katika
masumbwi zilikuwa zimefikia ukomo.
Mbabe huyo
amefuta wale waliokuwa na dhana hiyo baada ya kurejesha heshima yake kwa
kumchakaza kwa pointi Brandon Rios mjini Macau, katika pambano alilolifanya kwa
ajili ya kusaidi waathirika wa mafuriko yaliyotokea nyumbani kwao Ufilipino na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 4000 na wengine milioni nne wakikosa makazi.
Alishinda
kwa jumla ya pointi 120 kwa 109 na baada ya kumalizika kwa pambano hilo Pacquiao
alitamka bayana kwamba yuko tayari kupambana na bondia yeyote akiwamo mbabe
asiyepigika Floyd Mayweather.
Bob Arum ambaye
ni promota wa Pacquiao ametenga kiasi cha dola milioni 300 kwa ajili ya pambano
hilo lakini Mayweather ameshalitolea nje kwa kusema kuwa “sina mpango wa
kufanya kazi na promota huyo, kwa sababu ni mbabaishaji amekuwa akikataa kuweka
pambano hilo katika miezi ninayotaka ya May na Septemba,”.
USICHOKIJUA
Usichokijua
ni kwamba mwanasoka maarufu kutoka Uingereza, David Beckham amebainisha kwamba
ni shabiki mkubwa wa mbabe Manny Pacquiao na kwa kuthibitisha hilo hata katika
pambano lake lililopita alisafiri hadi Macau kwenda kumshangilia.
Jambo
jingine ni kwamba Manny Pacquiao amekuwa ni mpenzi wa hayati Bruce Lee na
amekuwa akipenda kuuweka mwili wake kama mpambanaji huyo wa zamani aliyejipatia
sifa kubwa duniani.
Kuingia
katika katika medani za siasa haikuwashangaza sana Wananchi wa Ufilipino kwa
kuwa alishaanza kukuzwa na rais wan chi hiyo, Arroya.
Mwaka 2012,
Pacquiao aliweka rekodi ya kushika nafasi ya pili ya kuwa mwanamichezo na
bondia anayelipwa zaidi duniani akilipwa dola milioni 62 huku nafasi ya kwanza
ikikamatwa Floyd ‘Money’ Mayweather.
Ukiachilia
masuala ya ngumi pia ni mwigizaji mzuri wa filamu akiwa amecheza tamthilia
kadhaa zinazoratibiwa na ABS-CBN
UTAJIRI
Mbabe huyo
anamiliki utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 100 (sawa na shilingi bil.
160).
Fedha hizo
amekuwa akiziingiza kwa mchezo wa ngumi na kufanya matangazo mbalimbali ya
kibiashara ikiwamo tangazo la bia za San Migue.
Ukiachilia
hayo mbabe Manny anamiliki baada yake kubwa katika maeneo maarufu kwa starehe
katika kisiwa Boracay huko Aklan akiwa ameshirikiana na mfanyabiashara
mwingine, Crisostomo ‘Cris’ Aquino waliyoianzisha tangu mwaka 2006.
Baa ya
wawili hawa inajulikana kwa jina la Boracay West Cove ikiwa
inakarabatiwa kila
mwaka kwa kufanya kuwa na muonekano mzuri na mpya.
NYUMBA
Mbabe huyo
anamiliki mjengo mkubwa nchini mwao, ikiwa na vyumba vya kulala saba, nyumba
hiyo iko kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,300.
Paa lake
limejengwa kwa vigae maalum kutoka nchini Japan ikiwa ni pamoja na geti la
kufunguliwa kwa rimoti.
Jumba hilo
lina bwawa la kuogelea ambalo lina sura ya glovu ya ngumi, kwa pembeni ya bwawa
hilo kuna vitu kwa ajili ya waogeleaji na wageni wa nyumba hiyo. Jumba hilo pia
lina gereji yenye uwezo wa kuhifadhi magari saba.
Bondia huyo
ametumia gharama kubwa za fedha kwa ajili ya kulifanyia ukarabati jumba hilo na
kuliwezesha kuwa na muonekano mzuri na wa kuvutia.
USAFIRI
Pamoja na
kwamba mbabe huyo amekuwa na magari mengi lakini amekuwa akipenda zaidi kutumia
gari aina ya Brand-new Ferrari 458 Italia.
MAHUSIANO
Jinkee
Pacquiao 2006, Ara Mina aliyekuwa naye tangu mwaka 2007 na Krista Ranilo
aliyedumu naye tangu mwaka 2009 hadi 2010.
Mbabe huyo
anaishi na mkewe anayejulikana kama Maria Geraldine Jamora na wamefanikiwa
kupata watoto wanne ambao ni Emanuel, Princess, Michael na Queen Elizabeth.
WASIFU
JINA:
Emanuel Manny Pacquiao
UMRI: Desemba
17, 1978
ENEO LA
KUZALIWA: Bukidnon, Mindanao, Philippines
KIMO: Futi 5
na inchi 6
UTAIFA: Ufilipino
No comments:
Post a Comment