Sunday, January 19, 2014

Burundi yafufua matumaini michuano ya CHAN 2014

.

http://www.yeswefoot.com/medias/burundi-team.jpg
Burundi
WAWAKILISHI wa CECAFA katika michuano ya CHAN 2014 inayoendelea Afrika Kusini, Burundi imefufua matumaini yake ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya muda mfupi uliopita kuicharaza Mauritania kwa mabao 3-2 na kuongoza kwenye msimamo wa kundi lao la D.
Ely Ould Voulany aliishtukiza Burundi kwa kuifungia Mauritania bao dakika ya pili ya mchezo huo kabla ya Abdoul Razak Fiston kusawazisha katika dakika ya 11 kutokana na kazi nzuri ya Suleiman Ndikumana, ambaye alifunga pia bao dakika ya 25 lakini lilikataliwa na mwamuzi na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Burundi kupata bao la pili lililofungwa na Nduwarugira katika dakika ya 61 akitengeneza pande na Fiston kabla ya Mauritania kusawazisha dakika ya 70 kupitia Demma kabla ya Ndikumana kufunga bao la ushindi dakika za nyongeza za pambano hilo na kuifanya Burundi kuiengua Gabon kileleni licha ya kulingana nao pointi nne ila wanatofautiana mabao ya kufungwa na kufungwa.
Kipigo hicho cha Burundi limeifanya Mauritania kuwa timu ya tatu kuaga mashindano hayo ikiungana na timu za Msumbiji na Ethiopia zilizotangulia mapema katika makundi yao.
Kesho mechi za lala salama za raundi ya tatu ya makundi hayo zitaanza kwa Nigeria kuvaana na wenyeji wao Afrika Kusini katika pambano la kundi A na Msumbiji kuvaana na Mali, mechi zote zikichezwa wakati mmoja majira ya saa 2 usiku.

No comments:

Post a Comment