Wednesday, January 29, 2014

KAMPUNI YA ISSERE SPORTS YATOA JEZI KWA SHULE YA SEKONDARI YA KEREZANGE


Mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo (Kushoto) akimkabidhi jezi namba 14 Mkuu wa Shule ya Sekondari Kerezange, Kivule Ilala Dar es Salaam, Bi. Kirundu Mgeni kwa niaba ya Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Isere kwa ajili ya timu ya soka shuleni hapo, Issere Sports ilitoa jezi mipira miwili na soksi (Picha na Mpigapicha Wetu) 

KAMPUNI ya kuuza vifaa vya michezo, Issere Sports imetoa jezi mipira na soksi kwa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Kerezange, iliyoko Kivule Ilala, Dar es Salaam.

Akikabidhi jezi hizo mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Issere, Abbas Ally alisema michezio inafanya wanafunzi kuondokana na maradhi.

Ufunguo aliyekubali kufundisha timu ya soka ya shule katika mashindano ya shule za Sekondari (UMISETA) alisema atatumia uwezo wake kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Mkuu wa Shule hiyo. Kirundu Mgeni alisema vifaa hivyo ni chachu ya wachezaji wa shule yake kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya wilaya yao ya Ilala.

Awali Mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Baraka Mololo alisema shule yake ina wachezaji wengi wenye vipaji ambao wakiendelezwa wanaweza kuchezea timu za Simba na Yanga na hata Taifa.

Alisema hivi karibuni shule hiyo ilifanya vizuri katika mashindano ya kirafiki na shule za jirani na kuibuka washindi hivyo ana matarajio makubwa ya kutwaa ubingwa wa UMISETA mwaka huu.

No comments:

Post a Comment