Wednesday, February 26, 2014

FAINALI YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA KUFANYIKA JUMAPILI HII MBEYA



Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania[TBL] Kanda ya nyanda za juu kusini, Claud Chawene amesema lengo kuu la mashindano hayo kuwa ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika utayarishaji na uchomaji wa nyama choma.

 Michael Machellah 

Baadhi ya waandishi wa habari



HOTEL YA MIKUYU ENEO AMBALO MKUTANO WA TBL ULIFANYIKIA


Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imefanikiwa kuwapata washiriki kumi waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano la nyama choma Mkoa wa Mbeya.
Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika Machi 2 Jumapili mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi  Ruanda Nzovwe.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania[TBL] Kanda ya nyanda za juu kusini, Claud Chawene amesema lengo kuu la mashindano hayo kuwa ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika utayarishaji na uchomaji wa nyama choma.
Chamwene ameyabainisha hayo alipokuwa anaongea na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Hoteli ya Mkuyu iliyopo Ilomba Jijini Mbeya ambapo awali washiriki walipatiwa mafunzo na wakufunzi mbali mbali ili kuyafanya mashindano hayo kuwa na ubora.
Amezitaja Baa zilizofanikiwa kuingia katika mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Jiji la Mbeya utakaofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe ni pamoja na Baa ya New city pub,Kalembo,Bonanza Bar,Blue House,Rombo Deluxe na Nebana.
Nyingine ni pamoja na Tarakea Bar,Savoy Bar,Mbeya City Pub na Iwawa ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja,wa pili shilingi laki nane,wa tatu laki sita,wa nne laki nne na wa tano atapatiwa shilingi laki mbili.
Aidha Claud amesema mpambano huo utahanikizwa na muziki wa bendi ya TOT ya Mbeya ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa kutoka kwa washabiki ambao wamepania kushuhudia shindano litakaloanza majira ya saa nne asubuhi.

                                                    Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment