Wakili
wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Angaza Mwaipopo akifafanua jambo
wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
Jaji
Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Crecensia Makuru akizangumza
jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati sherehe za siku
ya Sheria zilizofanyika leo.
Wakili wa kujitegemea Mary Munissi wa mkoani Dodoma akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo
Mahakimu,
Mawakili na watendaji wengine wa mahakama wakifuatila jambo walipokuwa
kwenye maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza jambo na Kaimu
mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mh.
Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za maadhimisho ya siku
ya sheria leo.
Na John Banda, Dodoma
UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi
mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na
upungufu mkubwa wa majaji. Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dodoma, Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.
Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.
Crecencia
alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni wachache kulingana na kesi
zilizopo ambapo hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya
mashauri na 1364 na kuna majaji wawili tu. Alisema ''idadi ya kesi ni kubwa mno kwa majaji wawili hii inachangia kwa kiwango kikubwa kesi kutosikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati, upo umuhimu wa kuongeza majaji ili kuwe na uwiano wa masharti yaliyopo'',
Aidha
alisema Mahakimu ni wachache huku mahakama nyingi za wilaya zina hakimu
mmoja mmoja licha ya kuwa na mashauri mengi na tatizo linakuwa kubwa
pindi mahakimu hao wanapougua, kuuguliwa au kwenda likizo. Aliongeza kuwa mahakama nyingi za mwanzo hazina mahakimu wa kudumu, mahakama hizo hutembelewa na mahakimu kutoka vituo vingine hali ambayo husababisha ucheleweshaji wa haki kwani mahakimu hulazimika kusafiri umbali mrefu na wakati mwingine miundombinu huwa ni mibovu..
Jaji huyo alibainisha kuwa sasa posho za washauri wa mahakama zimeboreshwa kutoka Sh.1,500 hadi kufikia 5,000 kwa kila shauri litakalohitimishwa. Alisema licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama kuna mikakati ya kutatua changamoto hizo ikiwemo kuondoa mashauri, kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili, kuboresha takwimu za mashauri, kesi zilizopo mahakamani, kuboresha na kusimamia masjala pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment