Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na
waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na
pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto
ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha
Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi.
Vicky Shayo.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAMILIKI Wote wa maeneo ya
biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa
wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la
umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti. Akizungumza
na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es
Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association
(Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo
wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa
zao.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake
wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la
DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na
Ubalozi wa Kenya nchini.
“hata kama mjasirimali mwanamke
ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo changamoto kubwa ni kupata eneo la
kuweza kuuza hiyo bidhaa yake aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,”
amesema Mrema
Mwenyekiti, Mrema amesema kuwa
chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Board
of External Trade (BET) na Small industrial Development Organization
(SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka mikoa yote Tanzania.
Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali
Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa
zenye ubora wa kimataifa.
Amesema kuwa Tancraft ni chama
cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa kutumia mali ghafi za kutoka
nchini kama vile nguo za batik, vikapu, minyaa, vitu vya
ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na usindikaji wa
aiana zote zikiwemo asali.
“malengo makuu ya chama yalikuwa
ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la pamoja kwa ajili ya
kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema
Amesema kwamba chama cha
wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es Salaam Free Market
ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya kufanya biashara zao
bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo ya Chang’ombe mikono.
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise
Judicate Mushi, akitoa maelezo ya bidhaa zake za mchai chai za aina
mbili black na green tea na mishumaa, amesema kwamba Green Tea ni mchai
chai wa kijani kabisa ambao umesagwa kwa matumizi bora kwa afya ya
binadamu
Amesema uzuri wa kinywaji hicho unaweza kunywa kikiwa cha
moto au baridi, mchai chai ni dawa ya kushusha sukari, homa, presha,
misuli na sumu za mwilini.
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise
Judicate Mushi akimuonjesha aina ya chai mmoja wa waandishi wa habari
kutoka kituo cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
Mjasiriamali Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer,
akizungumzia ubunifu wake wa mavazi na ujasirimali utengenezaji wa nguo
za wakinamama na wakinababa na Carpet za ngozi, viatu vya ngozi, vikapu
na Batiki. Fatuma amesema alianza biashara miaka karibu 12 iliyopita
katika biashara yake ya vitu vya asili vya kiafrika na changamoto kubwa
kwake ni kujitangaza. Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Mwananchi
Communications, Bi. Maimuna Kubegeya.
Maimuna Kubegeya akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Mjasiriamali Fatuma Amour kwenye jengo
la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi
karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo watakuwa hapo kwa muda wa mwaka
mmoja.
No comments:
Post a Comment