mshindi
 wa king’amuzi cha azam katika promosheni ya winda safari ya Brazili na 
Serengeti Bw Godbles Sehaba katikati akikabidhiwa zawadi yake  na meneja
 mauzo eneo la mabibo Bi Anna Gassembe (kushoto) na afisa mauzo Bi Anna 
Msonga (kulia).
Washindi
 wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti Godbles Sehaba 
(kulia)na  Karushe Mathias  (kushoto) wakiwa na nyuso za furaha baada ya
 kukabidhiwa zawadi zao za king’amuzi cha azam walizoshinda baada ya 
kuchezeshwa droo hiyo siku ya jumatano.
Washindi
 wawili wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti wamekabidhiwa 
zawadi zao jumamosi katika bar ya muleba iliyopo maeneo ya Mabibo Dar es
 Salaam, washindi hao Bw Godbles Sehaba na Karushe Mathias wakiwa na 
furaha walipokea zawadi hizo na kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti 
kwa kuwapa zawadi hiyo, wakiwa kama mashabiki wakubwa wa soka la 
nyumbani washindi hao wamefurahia kupata zawadi itakayowawezesha 
kuangalia ligi za mpira wa miguu ya nyumbani bila matatizo.
Meneja
 mauzo eneo la mabibo hilo Bi Anna Gassembe ambaye alikabidhi zawadi kwa
 washindi amehimiza watu kuendelea kunya bia ya Serengeti kistaarabu ili
 wajishindie zawadi. "zawadi bado ni nyingi na zawadi kubwa ya safari ya
 Serengeti bado haijatolewa kwa hiyo muendelee kushiriki zaidi ili 
mjipatie zawadi mbalimbali" alisema Anna.
promosheni
 ya winda safari ya Brazili na Serengeti inaendelea na washindi wanaweza
 kujishindia zawadi za simu aina ya samsung galaxy tab, king'amuzi cha 
azam, pesa taslimu shilingi 5000 na 10000, bia za bure pamoja na zawadi 
kubwa ya safri ya kwenda Brazili.
No comments:
Post a Comment