Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dr Jakaya Kikwete kushoto akimnadi Lowassa jimboni kwake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 |
Waziri Mkuchika (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukiodaima leo mjini Iringa
..................................................................................................................................................
HUKU
baadhi ya makundi yakiendelea kuibuka na kutoa kauli mbali mbali
dhidi ya waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kuwa ameanza kampeni za
Urais mapema , waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika amesema kuwa hajafanya utafiti wowote juu ya
Lowassa hivyo hawezi kuzungumzia chochote kama ni rushwa ama lah.
Waziri
mkuchika alitoa kauli hiyo mjini Iringa leo wakati akihojiwa wa
wanahabari mara baada ya kumaliza kutoka hotuba yake ya maadili na
Rushwa kwa watumishi wa umma katika kikao cha kamati ya ushauri (RCC)
cha mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo .
Kwani
alisema Taasisi ya kuzuiana na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini
imekuwa ikiwakamata watu na kuwafikisha mahakakani bila kuogopa
kiongozi ama mtu wa chini na kuwa utendaji wa taasisi hiyo umekuwa
ukiziongatia haki kwa kila mhusika.
Mkuchika mbali ya kugoma kulizungumzia suala la Lowassa bado alisema kuwa suala la Rushwa ni suala ambalo halikubaliki na kuziagiza
Halmashauri ya wilaya nchini kuchunguza mienendo ya watumishi
ambao waongoza kwa kumiliki mali mara baada ya kuingia serikalini ili kujua utajiri huo wa haraka wanaotoa wapi.
Hata
hivyo akihojiwa juu ya sakata ya aliyekuwa mshindi wa kura za
maoni ndani ya CCM katika mchakato wa ndani ya chama hicho mwaka 2010
Frederick Mwakalebela suala lake kuchukua muda mwingi zaidi na
kurudishwa mahakamani mara kwa mara alisema ili kuwa si kwa lengo la
kumuonea ila ilikuwa ni kutafuta sheria inasemaje katika hilo na
mahakani ndicho chombo pekee cha kutafsiri sheria hivyo maamuzi ya
mahakamani siku zote ni sahihi katika kutafuta haki.
Awali
Waziri Mkuchika akihutubia katika ufunguzi wa kikao hicho cha RCC
alisema kuwa mikakati ya ofisi yake katika kupambana na watumishi
wasio na maadili ambao wanashindwa kufanya kazi ya umma na kutumia
ofisi za umma kujinufaisha wenyewe.
Alisema
kuwa iwapo watumkishi wa umma hawatakuwa na maadili katika
uwajibikaji wao wa kila siku ni wazi suala la rushwa katika idara
wanazoongoza zitaendelea kuongezeka hivyo kuifanya jamii
kuendelea kuchukia serikali yao.
Hata
hivyo alisema ni vema Halmashauri kuhakikia kamati za maadili ya
watumishi zinafanya kazi vema ili kuwabaini watumishi wasio na
maadili katika Halmashauri zao.
Pia
alisema serikali kila mwaka imekuwa ikipelekea fedha zaidi ya
asilimia 70 kwa Halmashauri kwa ajili ya manunuzi ila matokeo yake
badala ya fedha hizo kutumika katika manunuzi wajanja wamekuwa
wakizitumia kujinunulia mali zao jambo ambalo alidai halitavumilika
katika wataki huu.
"
Haiingii akilini kuna mtumishi ameingia katika ajira akiwa hana
hata gari wala nyumba ila baada ya miezi miwili ya utumishi wa umma
unakuta ana nyumba za kisasa, magari na mali nyingi ambazo mazingira
ya upatikanaji wake yanatia shaka .....lazima kuwa makini sana na
maofisa ardhi na wakuu wengine wa idara "
Aidha
alisema katika kukomesha vitendo vya rushwa katika Halmashauri ya
idara mbali mbali za serikali amewaagiza makamanda wa taasisi ya
kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU ) kuhakikisha wanatoa
elimu kwa mabaraza ya madiwani wa Halmashauri zote nchini ili
kuhakikisha vitendo vya rushwa katika Halmashauri vinakomeshwa.
Waziri
Mkuchika alisema kuwa hadi sasa kwa nchi zinazoongoza kwa utawala
bora katika jumuiya ya Afrika Mashariki takwimu zinaonyesha kuwa
kati ya nchi tano Tanzania ni nchi ya pili kwa utawala bora .
Pia
alisema chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa mtumishi wa umma ni
pamoja na tamaa ya mali kwa watumishi hao hali inayosababishwa na
kutoridhika na kipato halisi wanachokipata pamoja na ubinafsi wa
kujitazama wao badala ya Taifa .
"Takwimu
kuhusiana na vita dhidi ya Rushwa na uwajibikaji kwa viongozi
unakabiliwa na changamoto nyingi..... takwimu kuhusiana na vitendo vya
Rushwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2012 hadi Juni 2013
zinaonyesha kuwa na jumla ya taarifa 81 zilipokelewa kati ya hizo 65
zilifanyiwa kazi uchunguzi na kufunguliwa majalada .....aidha katika
kipindi hicho jumla ya kesi mpya 12 zilifunguliwa katika mahakama mbali
mbali za mkoa wa Iringa na kesi 5 kati ya hizo zilitolewa hukumu na
wahusika kupewa adhabu mbali mbali" alisema waziri Mkuchika
Kuwa
Halmashauri ya wilaya pamoja na idara ya afya ndizo zinaongoza kwa
kuwa na taarifa nyingi kwa upande wa idara za serikali ambapo kila
moja ilipatikana na taarifa 16 huku idara ya mahakama inafuatia kwa
taarifa 6 wakati polisi na idara ya elimu zikiwa na taarifa 5 kila
moja idara ya maliasili taarifa tatu na idara ya mwisho kwa kuwa na
taarifa ndogo za rushwa ni idara ya ardhi na TANROADS ambayo ilikuwa
na taarifa moja ,Tanesco taarifa moja,SIDO mbili,ofisi ya mkuu wa
wilaya tatu ,na sekta binafsi taarifa tatu.
Mkuchika
alisema kuanzia sasa maofisa wa Takukuru wilaya ya mkoa hakuna
kushinda ofisini na badala yake kwenda kwa wananchi kutoa elimu ya
Rushwa na kuzitaka taasisi mbali mbali zikiwemo za dini kutosita
kutoa taarifa kwa Takukuru kuomba maofisa wake kufika na kutoa elimu
katika mikusanyiko.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephano Mhapa mbali ya
kumpongeza waziri Mkuchika kwa utaratibu wake wa kuzunguka katika
mikoa na kuzungumza katika vikao vya RCC bado alimshauri kufanya
mikutano ya hadhara kwa wananchi zaidi ambao ndio wanaathiriwa
zaidi na rushwa ndogo zinazoendelea kutolewa na kuvuruga ubora wa
miradi.
Huku
mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu alisema kuwa mbali ya
wilaya yake ya Mufindi kuongozana na maofisa wa TAKUKURU katika
mikutano yake wilayani ila bado inapaswa TAKUKURU kujipanga kwa
kutenga bajeti ya kufikisha elimu zaidi kwa wananchi.
Kwani
alisema iwapo TAKUKURU haitakuwana nguvu zaidi ya kuwafikia
wananchi wa pembezoni zaidi bado vita dhidi ya Rushwa itaendelea
kuzungumzwa pasipo kueleweka vema.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema Rushwa inayotesa wananchi ni ile inayotokana na
uwajibikaji mbaya wa viongozi wa serikali za vijiji na kata ambao
ndio wamekuwa wakiongoza kwa rushwa ndogo ndogo ambazo zinaendelea
kutesa wananchi .
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma aliwataka watumishi wote
wa umma na wananchi wa mkoa wa Iringa kushirikiana katika mapambano
dhidi ya Rushwa kama njia ya kuongeza kasi ya maendeleo katika mkoa.
Dr
Ishengoma alisema kuwa iwapo kila mmoja atajikita katika vita dhidi
ya Rushwa mkoa wa Iringa unaweza kuwa mkoa wa mfano kwa maendeleo
makubwa bila Rushwa
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Ishengoma aliagiza
Halmashauri zote za mkoa wa Iringa ndani ya miezi mitatu kuitisha
semina ya utawala bora katika suala la Rushwa na maadili kwa
madiwani wake.
"Mheshimiwa
waziri napenda kukuhakikishia kuwa tunaye kamanda wa TAKUKURU Mzuri
katika mkoa wa Iringa japo kamanda nakuomba usije kutia kiburi kwa
waziri wako kutokana na sifa hizi ambazo nimepata kukupa hapa
leo"
No comments:
Post a Comment