| Bondia Amani Bariki 'Manny chuga' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Moto wakati wa mpambano wao Many chuga alishinda kwa TKO ya raundi ya nne picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com | 
Bondia Kasimu Gamboo kulia akipambana na
 mohamed babeshi wakati wa mpambano wao Ganmboo alishinda kwa k,o ya 
raundi ya tatu ya mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
| REFARII OMARI YAZIDU AKIMWINUA MKONO JUU BONDIA KASSIMU GAMBOO | 
| bONDIA aLi Bugingo kushoto akioneshabna umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Mandula mandula alishinda kwa pointi | 
Bondia Fadhili Majia kulia akimtupia konde Juma Selemani wakati wa mpambano waio uliofanyika manzese majia alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu
Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
Bondia Iddi Bonge kushoto
 akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika 
manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika
 mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' 
mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka 
ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano
 wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam
mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi
 wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya 
mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi 
walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na 
filimbi
Bonge alipiga ngumi ya kwanza na 
kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na 
kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi 
hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi 
bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba 
ya uzito wa juu
mara baada ya mpambano huo bondia Iddi 
Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia 
Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono
 ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha 
mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina 
msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu
katika mpambano huo uliosindikizwa na 
mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally 
Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya 
raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma 
bondia  Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani 
akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia 
halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya 
kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point 
wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya 
raundi ya nne
Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa
No comments:
Post a Comment