Monday, March 17, 2014

Microsoft yawataka wateja wake waache kutumia Windows XP kutokana na ongezeko la Mashambulizi ya Virusi


windows xp
KOMPYUTA zinazotumia windows XP hazitoweza kupokea taarifa muhimu na kuongezeka mashambulizi ya virusi vya spyware vinavyoharibu taarifa binafsi na takwimu za kibiashara baada ya mwezi mmoja. Hayo yamebainishwa  jana  na Mkurugenzi wa Microsoft kwa kanda za Afrika Mashariki, Magharibi, Rotimi Olimide.

Alisema kuwa utafiti mpya wa Microsoft umeonyesha kuwa Window XP hushambuliwa kirahisi na virusi mara tano zaidi huku usalama wake ukiwa mdogo kiasi cha kuruhusu wizi wa mtandao.
  
Alisema ni vyema ndani ya mwezi mmoja, watumiaji wa window hiyo wakabadilika na kuhamia Window 8 ambayo ina uwezo mkubwa wa kuhimili mshambulizi ya virusi.
  
“Mfumo uliotengenezwa kwenye Window XP ni wa kizamani na uendeshaji wake sio iliyoundwa kujilinda dhidi ya virusi.
  
“Baada ya mwezi mmoja si kuwa huduma ya Window XP haitafanya kazi, unaweza kuendelea nayo lakini usalama na utendaji wake hautakuwa mzuri ,” alisema.
  
Alisema mfumo wa uendeshaji wa Windows 8 na Office 365 unatoa ulinzi wa uhakika na ufanisi. Mkurungezi wa Teknolojia na Uendeshaji, Chege Thumbi alisema ni vyema hasa taasisi za kifedha kuacha kutumia windows XP mara moja ili kuwa katika usalama na urahisi wa kufanya biashara.

No comments:

Post a Comment