Sunday, March 23, 2014

WANAFUNZI WANAWAKE CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR WAWEKA HISTORIA, WAANZISHA MFUKO WA KUWAKOMBOA KIELIMU.



Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (kulia) akizungumza  na wanafunzi wa Kike wa chuo cha CBE kampasi ya Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu.
 Baadhi ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakifurahia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu, kisiasa na kiutamaduni leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Kike wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (katikati). Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

========  ========  =========
WANAFUNZI WANAWAKE CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR WAWEKA HISTORIA, WAANZISHA MFUKO WA KUWAKOMBOA KIELIMU.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
22/3/2014. Dar es salaam.

Wanafunzi wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wamezindua mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya wanafunzi wa kike wenye lengo la  kumkomboa na kumwezesha mwanafunzi wa kike kujitambua, kielimu, kisiasa na kiutamaduni.

Akizungumza na jumuiya ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakati wa uzinduzi  wa mfuko huo  leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mery Mwangisa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo  ni ishara ya umoja na mshikamano wa wanafunzi wa kike chuoni hapo.

Amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kunatokana na kuongezeka kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake pia  kukosekana kwa mifuko ya aina hiyo katika taasisi nyingi za elimu ya juu hapa nchini.

Ameeleza kuwa  malengo ya mfuko huo ni kumwezesha mwanafunzi wa kike wa CBE kujitambua kielimu, kisiasa na kiutamaduni na kuongeza kuwa yamekuja  wakati muafaka kufuatia  mabadiliko yaliyopo sasa ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.

 Amefafanua kuwa mfuko huo ulioanzishwa katika chuo hicho ni fursa pekee ya kuwawezesha wanafunzi wa kike kunufaika kwa kupata elimu bora bila vikwazo.

“Napenda kutumia fursa hii kuushukuru uongozi wa chuo hiki kwa kuonyesha njia ya kuwajali wanawake na pia katika kuweka taratibu nzuri za kulinda maadili, katika maisha yangu sijawahi kusikia chuo kikuu chochote kimezindua jukwaa la wanawake lenye malengo mazuri kama yenu” Amesema Dkt. Mwangisa.

No comments:

Post a Comment