Sunday, April 13, 2014

Mvua yapeperusha pambano la Miyeyusho, Cheka PTA


Miyeyusho na mpinzani wake juzi walipopima uzito kabla ya mechi yao kuahirishwa jana kwa sababu ya mvua
MVUA kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam, limesababisha kulipeperusha pambano la ngumi la kimataifa kati ya mabondia wa Tanzania, Francis Miyeyusho dhidi ya Mthailand Sukkasem Kietyngyuth lililokuwa lifanyika usiku wa jana kwenye ukumbi wa PTA.
Siyo pambano hilo tu, bali hata pambano jingine la kimataifa baina ya bingwa asiyepigika nchini, Francis Cheka dhidi ya Gavad Zohrehvand wa Iran nalo lilishindwa kufanyika kwa sababu hizo hizo na sasa waratibu wanajipanga kutangaza tarehe mpya, japo imedaiwa michezo hiyo itachezwa mwishoni mwa wiki hii.
Waratibu wa michezo hiyo isiyokuwa ya ubingwa iliyoandaliwa chini ya Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) walitangaza kuahirisha pambano hilo majira ya saa 1 usiku baada ya kutishwa na mvua iliyokuwa imejesha kutwa nzima ya jana bila kukoma.
Hata hivyo mvua hizo zilikoma majira ya saa tatu wakati mashabiki wakiwa wameshatawanyika na hivyo kujipanga kuangalia namna michezo hiyo ifanyike lini ili kuzima kiu ya mashjabiki waliokuwa wana hamu ya kuona mabondiawa Tanzania wangefanya nini dhidi ya wageni hao.

No comments:

Post a Comment