Sunday, April 13, 2014

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAINGIA SIKU YA PILI MKOANI DODOMA, MCHUJO KUANZA KESHO


Mmoja wa washiriki wa Shindano la kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania, lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) Bw Stephen Mapunda  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kwa zoezi la usaili katika shindano la TMT.
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya Kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji wakiwa katika mstari tayari kwa kupewa fomu ya usaili ili kuweza kushiriki kwenye shindano la TMT.
 Baadhi ya washiriki waliofika katika ukumbi wa African Dream kwaajili ya usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya shindano hilo ambalo kwasasa linaendelea Katika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma.
Kundi la kwanza likiwa tayari kwaajili ya kupewa namba za ushiriki mara baada ya kumaliza zoezi zima la kujaza fomu za ushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mkoani Dodoma leo ikiwa inawakilisha Kanda ya Kati.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.

Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.

Shindano la Tanzania Movie Talents leo limeingia siku ya pili ya usaili mkoani Dodoma, Kanda ya Kati ikiwa na washiriki waliojitokeza zaidi ya 600. Shindano hili limeibua hisia za Watu wengi kutokana na Umahiri wake na kuwa shindano la kwanza kutokea Afrika Mashariki na Kati huku maandalizi yake yakiwa yamefanyika kwa umakini wa hali ya juu huku Majaji wa Shindano hilo wakitokea kuwa Vivutio vikubwa kwa washiriki hao kutokana na jinsi wanavyotoa Uamuzi.

Washiriki zaidi ya 600 wameweza kujitokeza kushiriki shindano hili ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na mpaka sasa zoezi hili limeingia siku ya pili ambapo timu ya TMT imeendelea kusaili vijana waliojitokeza.

Safari ya Mchujo wa shindano hili kwa kanda ya kati ambapo shindano hili linafanyika mkoani Dodoma utaanza kufanyika kesho Jumatatu ili kuweza kupata washindi watatu bora ambao kila mmoja atajiondokea na Kitita cha Shilingi laki tano (500,000) kwa kila mshindi na baadae kujiunga na washindi wengine wa kanda zilizobakia Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na kupelekea Mshindi kujinyakulia zawadi kubwa kabisa ya Kitita cha pesa za Kitanzania Milioni 50 (50,000,000/=) na vilevile washindi kumi bora katika fainali hiyo watakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions na watafanya kazi ya pamoja na hatimaye kazi yao kuweza kuuzwa nchini nzima na wao kunufaika na kazi hiyo.

Shindano hili linaloendelea kufanyika mkoani Dodoma linatarajiwa kumalizika mnamo Jumanne ya 15 April 2014 na siku hiyohiyo Washindi watatu watatangazwa.

Baada ya shindano hili kumalizika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, shindano litaelekea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya kwaajili ya vijana kuweza kuitumia fursa hii kwaajili ya kuonyesha Uwezo na vipaji vyao katika Kuigiza.

Katika Shindano hili vijana wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuitumia fursa hii na hatimaye kuweza kuonyesha vipaji vyao kwa maana huu ndio muda wao.

Hakuna viingilio katika shindano hili na fomu zinapatikana bila gharama yoyote ile.

No comments:

Post a Comment