Thursday, April 10, 2014

WASANII WA FILAMU WAKUTANA KUJADILI MUSTAKABALI WA FANI HIYO NCHINI.


Steve Nyerere akifafanua jambo

Wadau wa filamu wakifuatilia mjadala huo kwa umakini
Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisoo akifuatilia jambo katika mjadala huo,


WASANII na filamu wametakiwa kutengeneza filamu zenye kuendana na maadhi ya kitanzania ikiwa pamoja na kutangaza uzuri wa nchi ya Tanzania.

Pia wametakiwa kutumia DVD na CD zenye ubora unaoweza kuhifadhi kwa muda mrefu filamu zao.

Wito huo ulitolewa jana na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga wakati akifungua mkutano ulioshirikisha wadau wa filamu nchini kwa lengo la kujadili mustakabali wa fani hiyo.

Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Taifa, Sihaba aliwataka wadau hao kujadili kwa kina suala zima la mikataba kandamizi kwa wasanii ikiwa pamoja na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kutatua kero hiyo.

Sihaba pia alisema kuwa kupitia kikao hicho ndio kitatoa mwanga kwa serikali kupitia Wizara yake kutafuta mwafaka wa kero zao mbalimbali.

"Kupitia mjadala huu ndio serikali itajua mengi mfano mzuri ni suala zima la bei elekezi inayotakiwa kutumiwa katika kuuza filamu zenu, sasa basi mtumie vema mijadala kama hii kutupatia mwanga wa nini tunachotakiwa kufanya ili kuwasaidia"alisema Sihaba.

Katika kikao hicho cha kujadili mustakabali wa soko la filamu mwenyekiti wa Bongo Movie Steven Nyerere alisema kuwa mbali na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo zipo ambazo zingepaswa kuwa zimeshatatuliwa hadi sasa.

Alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia suala zima la uharamia katika kazi za filamu huku kukiwa hadi sasa hakuna hatua madhubuti inayochukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Alisema kuwa hiyo inaathiri mustakabali mzima wa filamu hapa nchini kwa kuwa wasambazaji wanashindwa kufanya kazi zao kwa faida.

Pia aliitaka serikali kuhakikisha kuwa inawawezesha wasanii kuigiza filamu zao hata katika maeneo nyeti kama vituo vya polisi.


"Ndio maana filamu zetu yabi ni pale pale kama msanii akiigiza chumbani akitoka yupo sebuleni au mtaani au baa yani kunakuwa hakuna utamu wa uigizaji wenyewe sasa kwa nini tusiigize hata katika vituo vya polis kwa mfano"alihoji Nyerere.

No comments:

Post a Comment