Bi
 Regina Gwae ( wapili kushoto), Akiongea na wana habari kwa niaba ya 
kamati ya maandalizi ya Nice and lovely jijini Dar es Salaam kuhusu 
shindano la miss Tanga linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 
katika ukumbi wa Mkonge hotel (watatu kulia),Meneja Mauzo Nice and 
lovely Bw.Brian Kelly.
 waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Bi
 Regina Gwae (kushoto),akiwaonyesha waandishi wa habari gari lenye 
thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely  litakalo shindaniwa katika shindano hilo (kulia), meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw.Brian Kelly.
========  ====  ======
Wito
 umetolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa
 wingi kushuhudia shindano kubwa na la aina yake la kuwania taji la 
ulimbwende linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi 
wa Mkonge hotel.
Akiongea
 na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely Bi 
Rejina Gwae amesema kuwa wanajivunia kupata nafasi ya kuwa waandaji wa 
shindano hilo na kutoa wito kwa warembo wote wenye nia ya kushiriki 
kujitokeza kwa wingi.
Kuhusu
 zawadi kwa mshindi Bi Rejina amesema kuwa mshindi ataondoka na gari 
lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely
 akasema kuwa pia kuna zawadi nyingine za pesa taslimu toka kwa washindi
 wengine ambazo wanatarajia kuzitangaza baadae.
Kwa
 upande wake meneja mauzo wa Loreal  wamilikiwa wa bidhaa za Nice and 
lovely Briyan Kelly alianza kwa kuishukuru kampuni ya Mac D promotion 
kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wa nafasi hiyo na kuahidi kuitendea 
haki nafasi hiyo.
Akamalizia
 kwa kutoa wito kwa wote wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo 
kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana 
Mkonge hotel, D,boutique tanga mjini,Breez fm,Tanga beach resort, Five 
brothers, Mwambao fm, Sophia records, Danny fashion barabara ya 13, 
ofisi za the guardian tanga barabara ya 15 na  Yolanda salon mtaa wa 
Eckenford na Nyumbani hotel.



No comments:
Post a Comment