Kituo
cha radio cha 100.5 Times Fm, June 21 kilitoa mchango wa vifaa
mbalimbali kwa ajili ya kukisaidia kituo cha polisi cha Kawe, wilaya ya
Kinondoni, Dar es Salaam.
Times
Fm imetoa mchango huo baada ya kubaini changamoto mbalimbali za
kiutendaji zinazokikabili kituo hicho cha polisi kutokana na upungufu wa
vifaa.
Baadhi
ya vifaa vilivyokabithiwa kwa kituo hicho cha polisi ni pamoja na viti,
meza na vifaa mbalimbali vitavypotumika katika uandishi na uchapaji wa
taarifa zao (Stationary).
Akizungumza
kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Camilius
Wambura, Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Kawe SSP Mponjoli, aliushukuru
uongozi wa kituo hicho kwa hatua walioichukua na kukitaja kama mfano wa
kuigwa kwa jamii, vituo vingine pamoja na mashirika mbalimbali katika
kutambua kuwa kuisaidia polisi ni kuisaidia jamii.
Alisema
vifaa hivyo vitawasaidia sana katika kurahisha utoaji wa huduma kwa
jamii kwa kuwa wamekuwa na changamoto ya upungufu wa vifaa hata kufikia
hatua ya kuwaomba wananchi wanaohitaji huduma kujinunulia vifaa kama
karatasi za kuandikia taarifa zao.
“Zamani
watu walikuwa wanaona vituo vya polisi kama adui. Lakini hivi sasa ni
wakati ambao watu wanatakiwa kuachana na fikra hizo potofu na
kuvichukulia vituo vya polisi kama marafiki kwa sababu polisi ni sehemu
ya jamii. Jamii inaitegemea polisi na polisi wanaitegemea jamii. Times
Fm mmeonesha mfano wa urafiki kwa kusaidia, tunawashukuru sana. Nyie ni
mfano wa kuigwa kwa jamii na mashirika mengine.” Alisema Mponjoli.
Naye
mkurugunzi wa Times Fm Radio, Rehure Nyaulawa alitoa wito kwa makampuni
na watu mbalimbali kudumisha amani na usalama na kuisaidia polisi kama
sehemu ya jamii .
“Sisi
tunaamini kwamba polisi hawako mbali na jamii, shughuli za kipolisi na
jamii zinaenda pamoja. Kwa hiyo sisi tutaendelea kuzunguka tukifanya
michezo na kuisaidia jamii kadiri tunavyoweza na sio polisi pekee.
Hatuwezi kumaliza matatizo lakini tunatoa tunachoweza na tutakuwa kama
mfano kwa wengine pia kuweza kujitolea.” Alisema Rehure Nyaulawa.
Wiki
mbili zilizopita Times Fm ilitoa mchango wake kwa chama cha Albino
Temeke ili kusaidia kundi hilo kupambana na changamoto za mahitaji
zinazowakabiri.
Michango
hiyo hutanguliwa na mechi za kirafiki za mpira wa miguu kati ya timu ya
Times Fm (The Dream Team) na timu ya wakaazi wa eneo husika.
Mkurugunzi
Mkuu wa Times Fm Radio, Rehure Nyaulawa (kushoto) akikabidhi kwa Mkuu
wa Polisi wa Wilaya ya Kawe, SSP Mponjoli,sehemu ya mchango wa vifaa
mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kukisaidia kituo cha polisi cha
Kawe, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pongezi mara baada ya makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment