Wednesday, June 25, 2014

CHADEMA KWAWAKA, WAJUMBE WAKE WA BARAZA KUU NA WANACHAMA WATINGA KWA MSAJILI WA VYAMA NA KWA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUOMBA MBOWE NA SLAA WADHIBITIWE KWA UFISADI


 Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
 Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama
 Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
 Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
 Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
 Yona akionyesha abarua ambayo baadaye aliikabidhi masijala kwa ajili ya kumfikia Msajili wa vyama
 Yona akikabidhi barua yao, kwa Mtunza kumbukumbu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa vyama, Jihadhari Saidi.
 Yona akizungumza nje ya Ofisi ya Msajili baada ya kuacha barua yao kwa Msajili wa Vyama
  Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo akisoma taarifa yao kabla ya kwenda kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baadaya ya kutoka kwa Msajili ya vyama
 Baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Chadema wakiwa na mabango nje ya Ofisi ya Msajili wa vyama
 Mamilioni ya ruzuku yanayeyukia wapi? Bango linauliza
 Eti Bora Chadema ife kuliko Mbowe kutapeli?
 Chadema wakiomba msaada kwa Msajili wa vyama
 Ujumbe mzito kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
   Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakiwa nje ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo kupeleka maombi ya kutaka Mkaguzi huyo wa Hesabu za serikali kufanya ukaguzi wa hesabu wa Chadema kwa madai kwamba viongozi wa ngazi za juu wanazitafuna


No comments:

Post a Comment