Tuesday, June 24, 2014

Mashindano ya pool - Mwanza

Na: Henry Kavirondo – Tarehe 23.6.2014 – Mashindano ya Pool – Mwanza.
Kikosi cha timu ya Biriadi Pool Table ya mkoani Mwanza kinatarajia kuuwakilisha mkoa wa Mwanza katika michuao ya Pool ngazi ya Taifa baada ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ngazi ya mkoa wa Mwanza baada ya kuibuka na Pointi 13 kwa 11 dhidi ya Wanyama.
Reportage: Henry Kavirondo – Mwanza:………………………………………………………......
Katika mchezo huo kila ilikuwa imejidhatiti kutwaa ubingwa huo, lakini jitihada za mchezo zilizoonyeshwa na kikosi cha Biriadi Pool Table, ndizo zilizowawezesha kutengeneza historia ya kutwaa ubingwa huo msimu huu dhidi ya Wanyama.
Kutokana na matokeo hayo timu hiyo pamoja Mwanadada Rukia Issa, aliyefanikiwa kutwaa ubingwa kwa upande wa wanawake watauwakilisha mkoa wa Mwanza katika michuano hiyo ngazi ya Taifa inayotarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro baadaye mwaka huu.
(1)   BEKA MBULA – Nahodha wa timu ya Biriad Pool Table.
(2)   EMMANUEL GOYA – Nahodha wa timu ya Wanyama.
Mratibu wa michuano hiyo Michael Machela amewaambia waandishi wa habari kuwa tayari maandalizi yote ya michuano hiyo yameshakamilika ambapo jumla ya timu kutoka mikoa 17 nchini zinatarajia kushiriki katika michuano hiyo.
(3)   MICHAEL MACHELA – Mratibu wa michuano ya Pool Table kitaifa.
(4)   BENARD NAOMWISALIA  - Mwakilishi wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL).
Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imejikita kudhamini michuano ya Pool Table ngazi ya taifa ili  kuinua kiwango cha mchezo huo kimataifa lengo ikiwa ni kufungua milango ya ajira kwa vijana.

No comments:

Post a Comment