Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akikabidhi mchango wake wa Tsh
700,000 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za vicoba jimboni ……………………………………………………………………….. Na Francis Godwin Blog.
WANACHAMA
wa vikundi vya Vicoba Igunga na Amkeni Group kata ya Mgama katika
Halmashauri ya Iringa wamempongeza mbunge wa jimbo la Kalenga
Godfrey Mgimwa kwa kuviwezesha vikundi hivyo mtaji kwa ajili ya
kuwawezesha wanachama hao kukopeshana zaidi.
Mratibu
wa Vicoba mkoa wa Iringa Thisiana Kikoti alitoa pongezi hizo leo
wakati uzinduzi wa Vicoba katika kijiji cha Ihemi .
Kikoti
alisema kuwa uanzishwaji wa vikundi hivyo ni jitihada za aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega ambae alihamasisha
kuanzishwa kwa VICOBA mkoani Iringa na katika jimbo la Kalenga hamasa
ya kuanzishwa kwa vikundi hivyo imefanywa na aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa na sasa jitihada zinazofanywa na
mbunge wa sasa Godfrey Mgimwa ni wazi zitafanikisha kukua kiuchumi
kwa wananchi wa jimbo hilo.
Alisema kuwa lengo ni kuona inaanzishwa bendi ya VICOBA kwa ajili ya kuwawezesha wananchi zaidi kiuchumi. Huku
kwa upande wake mbunge Mgimwa mbali ya kuchingia kiasi cha Tsh
700,000 pia alisema kuwa ndoto ya mbunge aliyefariki wa jimbo hilo
ilikuwa ni kuanzisha benki ya maendeleo katika jimbo la kalenga na
kuwa tayari alianza kuandika andiko na suala hilo ataliendeleza .
wakati
huo huo mbunge huyo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi
700,000 kwa vikundi vya Ihekima ,tugele na Imani vyenye wanachama 80
kwa ajili ya kuviwezesha zaidi
vikundi hivyo vina akiba ya shilingi milioni 8 toka vilipoanmzishwa mapema mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment