Wednesday, June 4, 2014

MFUKO WA UWEZESHAJI WA WANANCHI ZANZIBAR WAWATUNUKU HUNDI ZA MIKOPO WAJASIRIAMALI


Mwakilishi wa Kikundi cha wajasiriamali wa usafirishaji abiria kwa njia ya Bahari cha Rehema za Mungu cha Kisiwa cha Tumbatu  Wilaya ya Kaskazini “ A “ akipokea hundi ya shilingi Milioni 2,400,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar..
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi 12 vya wajasiri amali wa Kisiwa cha Unguja wakifuatilia hafla ya utowaji Mikopo kwa vikundi vyao kutoka mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Mwanakwerekwe.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************
Vikundi 12 vya wajasiriamali wa miradi tofauti ya Maendeleo katika Wilaya sita za Kisiwa cha Unguja wamekabidhiwa hundi za mikopo kutoka Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi ulioanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Mfuko huo wenye lengo la kuwakomboa Wananchi hasa wanawake, Vijana pamoja na wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya sekondari na Vyuo ulizinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein Tarehe 21 mwezi  Disemba mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment