Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, George Mpondela kilichotokea jana
(Juni 15 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar
es Salaam.
Kwa
mujibu wa klabu ya Yanga, Marehemu Mpondela anatarajiwa kuzikwa
Alhamisi (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, na msiba upo
Kigamboni Mnarani.
Mpondela
alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga katika uchaguzi
uliofanyika mwaka 1994 baada ya kumshinda aliyekuwa mpinzani wake wa
karibu George Ndaombwa.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Mpondela
enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi katika klabu yake
ya Yanga.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mpondela, na klabu ya Yanga na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito.
Taratibu
zaidi za mazishi zitatolewa na Yanga baada ya kufanya mawasiliano na
familia ya marehemu Mpondela. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake
lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment