Monday, June 16, 2014

SHINYANGA KUMPATA MISS REDD’S 2014, JUNI 28. MJINI KAHAMA.


MRATIBU wa Shindano la Redd's Miss Shinyanga 2014,Asela Magaka aliyesimama akitoa neno katika uzinduzi wa kambi ya warembo iliyo katika Hotel ya Ihesa mjini Kahama,kushoto kwake ni Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Julius Kambarage na Mwakilishi kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ambao ni miongoni wa Wadhamini wa Shindano hilo,na kulia kwa Asela ni Mkurugenzi wa Ihesa Hotel;Ismail Luge. (Picha na Ali Lityawi)
NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014.
NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014.
Katika poz.
Kama kawaida mambo ya mitembeo yao.
NI Warembo waliongia kambini katika Hotel ya Ihesa iliyopo mjini Kahama tayari kuwania taji la Redds Miss Shinyanga 2014 wakionyesha dance.
Hapo vipi....!!
SHINYANGA KUMPATA MISS REDD’S 2014, JUNI 28.
MKOA wa Shinyanga unatarajia kumpata Mrembo wake “Miss Redd’s Shinyanga 2014”katika Kinyang’anyiro kitakachofanyika Juni 28,mwaka huu baada ya Walimbwende 20 wenye haiba kuingia kambini katika Ukumbi wa Ihesa Hotel &Resort Ltd ya mjini Kahama.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Asela Promotion inayoratibu wa shindano hilo Asela Magaka alisema tayari maandalizi ya awali yameanza ambayo ni kuwaweka kambini jumla ya warembo 20. ,kujifua ili kutwaa taji hilo.
Alisema warembo hao wamepatikana kutoka katika michuano ya urembo kutoka Wilaya sita za Mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Kahama, Shinyanga Mjini, Msalala Shinyanga Vijijini na Ushetu,huku wakiwa na mvuto mkubwa na viwango vinavyofafana hali ambayo italeta ushindani mkubwa miongoni mwao.
Magaka alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika tarehe 28/6/2014 katika ukumbwa Kisasa maarufu na mpya wa Shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) Mjini Kahama na kuwataka mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani anatwaa taji laMrembo wa Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu huyo alisema kuwa katika shindano hilo linatarajiwa kupambwa na Wasanii kutoka ndani na nje ya nchi wakiongozwa na mfalme wa Taarabu Nchini Mzee Yusuph, Amani kutoka Kenya na Mo Music.
Aidha aliwataja wadhamini wa Shindano hilo kuwa ni SSCN TV ya Mjini Kahama, Nonema Investiment, Trixie Social Media Market, Nyamizi Secretarial Service, Royal Supermarket, NSSF, Coca Cola, Redds na Global Publisher.
Wengine ni pamoja na Clouds FM, Three Jays’s Inverstment, CXC Africa, Williamson Diamond, Saluti, Ihesa Hotel, Kahama Commonity Health Dispensary, Tulliz Fashion, Ngeleja Gold Mine, Kahama Motel, Charitk Pub, Glory Pads na Barrick Buzwagi.
Mratibu huyo pia alisema kiingilio katika shindano hilo kinatarajiwa kuwa shilingi 60,000 kwa watu wa jukwaa maalumu ( VIP) wakati shilingi 20,000 kitakuwa ni kwa watu wa jukwaa la kawaida.

No comments:

Post a Comment