Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mwa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib
Bilal, Mkewe Mama Zakhia Bilal, Rais wa Burundi Mhe. Piere. Nkurunzinza,
na baadhi ya viongozi wa meza kuu, wakisimama kupokea maandamano ya
maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana katika
uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.
Rais
wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya
maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika katika
uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.
Rais
wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza, akisalimiana na mke wa Makamu wa Rais wa
Tanzania, Mama Zakhia Bilal, walipokutana kwenye Uwanja wa Prince Louis
Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa
Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza walipokutana
kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati
wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika jana.
Burudani kutoka kwa vikundi vya Burundi.....
Ujumbe
wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal
kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika leo
Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura
Burundi. Picha na OMR
****************************************
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA SIKU YA UHURU WA BURUNDI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo Jumanne Julai Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za
kilele cha miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika
Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.
Katika
sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia kulikuwa na
Makamu wa Rais wa Somalia, Waziri Mkuu wa Chad na viongozi mbalimbali
waliowakilisha nchi kutoka Afrika. Sherehe hizo zilianza kwa Rais Pierre
Nkurunzinza kuweka silaha katika eneo maalum la Uhuru na kufuatiwa na
maadhimisho yaliyoshirikisha wananchi mbalimbali katika uwanja wa
Rwagasore.
Akizungumza
baada ya kutoa tuzo mbalimbali za heshima, Rais Nkurunzinza
aliwashukuru wageni wote waliofika katika sherehe hizo na akabainisha
kuwa Tanzania ni rafiki wa Burundi hivyo anafurahishwa sana kuona ikiwa
imewakilishwa na uongozi wa ngazi za juu katika sherehe hizo.
Burundi
ambayo inategemea sana bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na hasa uwepo
wa Ziwa Tanganyika ambalo linaiunganisha na Tanzania, inaadhimisha miaka
52 ya uhuru huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali kiuchumi sambamba na
kisiasa kufuatia kuwa na miongo kadhaa ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa sasa Burundi licha ya kukua kimaendeleo pia inaongezeka idadi
ambapo inakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Uhusiano baina ya Tanzania na
Burundi unabaki kuwa wa damu ambapo pia redio za nchi hii hutangaza
vipindi kadhaa kwa kutimia Kiswahili sambamba na nyimbo za muziki za
wasanii wa Tanzania hupata nafasi kubwa katika redio za Burundi.
Katika
sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma
Maalim.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai Mosi, 2014 Bujumbura: Burundi
No comments:
Post a Comment