
Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa 
polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na 
wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali 
kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha 
vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali 
yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya 
ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo
 zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa 
fedha  kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa 
ambavyo  thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni
 Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani  ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya 
makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi 
Chalinze.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi 
mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na 
mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la 
Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. 
Magomi.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili 
kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na 
jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya 
kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.

 Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete  akimsikiliza Kamanda
 wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa 
akitoa shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara 
baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa  ituo cha 
polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa
 shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa 
akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la 
kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.

Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.

Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.

Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete  akisalimiana na wanafunzi 
wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua 
ujenzi wa shule hiyo.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi 
wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze 
Bw. Ahmed Nasser.

Mbunge
 wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya
 shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser
 mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla  kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.

Diwani
 wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbune 
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la 
polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
No comments:
Post a Comment