Thursday, July 3, 2014

MFARANSA SEAN GARNIER AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI HUKU AKIBINUKA SARAKASI NA KUCHEZA DANSI



 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.

 
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
  Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment