Akitoa
hotuba ya iliyo kuwa na historia ndefu ya klabu ya Simba, waziri Nkamia
alitumia fursa hiyo kuwataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa kitu
kimoja katika kipindi hiki kwa lengo la
kuendeleza mambo mazuri na yenye mafanikio.
Nkamia
amesema endapo wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo watashindwa
kutimiza wajibu wao wa kuipenda klabu yao na kuithamini, kuna
hatari kubwa ya kukosekana kwa historia nzuri kwa miaka ijayo.
Hata
hivyo Nkamia amempongeza muandishi wa kitabu hicho Mwina Seif Mohamed
Kaduguda kwa kutumia ujasiri wake kwa kuweka kumbukumbu mbayo
katu haiwezi kufutika.
Kwa upande mtunzi wa kitabu hicho Kaduguda ambaye aliwahi kuwa katibu wa klabu ya Simba amesema ameamua kufanya
hivyo kutokana na wanachama na mashabiki wengi kutokuijua vyema historia ya
klabu yao.
Amesema kwa mfumo wa kuyaandika mengi mazuri ya klabu ya
Simba alioutumia kuna kila sababu kwa kizazi cha sasa na kijacho kuona mwanzo
wa klabu hiyo mpaka ilivyo sasa na nini matarajio yake.
No comments:
Post a Comment