Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa 
mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba
 la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha
 Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga 
kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika 
vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano 
ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na 
kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya 
Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais 
alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, 
wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la 
Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa 
Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister 
Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma(picha na 
Freddy Maro)

No comments:
Post a Comment