Mratibu
wa Ziara ya Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Real Madrid,Ssebo (wa tatu
kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
mechi ya kirafiki kati ya Tanzania Eleven na Timu ya Wachezaji wa Zamani
wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho.Mpaka
sasa ni wachezaji watatu tu ndio waliowasili nchini huku wengine kadhaa
wakitegemewa kuwasili mchana wa leo.Wachezahi hao ambao wapo nchini hivi
sasa ni Luis Figo (wa tatu kulia),Christian Karembeu (kulia) na Beki
Fernando Sanz Duran (wa pili kushoto).wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya TSN,Farough Baghoza na Kocha wa Timu ya Tanzania
Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio"
Kocha
wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati)
akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili Wakali hao wa soka
Duniani wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye
Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Luis Figo na
kushoto ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya
Real Madrid ya nchini Hispania.
Mchezaji
Kiongozi wa Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo
akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ujio wao hapa nchini.Figo
amewaahidi wa Tanzania kuwa yeye na Wenzake watatoa burudani kabambe
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar hapo kesho.
Mchezaji Fernando Sanz Duran (kati) nae akitoa maneno yake kuhusu mchezo huo.
Mwanasoka Christian Karembeu akizungumza.
No comments:
Post a Comment