Na Anna Nkinda – Maelezo, Washington
Rais
wa zamani wa Marekani George W. Bush amempongeza Mke wa Rais Mama
Kikwete kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kuhamasisha jamii na
wanawake kwa ujumla kujitokeza kwa ajili ya kupima saratani ya matiti na
mlango wa kizazi.Pongezi
hizo zilitolewa jana na Rais huyo mstaafu ambaye pia ni mwanzilishi wa
Taasisi ya George W. Bush wakati akifungua mkutano wa wake wa Marais wa
Afrika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kituo cha Kennedy
(Kennedy Center) kilichopo mjini Washington.Mzee
Bush alisema Taasisi yake inasimamia mradi wa upimaji wa saratani ya
matiti na mlango wa kizazi, ili nchi za Afrika ziweze kupunguza idadi
ya wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na hadi sasa zaidi ya wanawake
100000 wamefanyiwa uchunguzi katika nchi za Tanzania, Zambia na
Botswana lakini tatizo lililopo ni unyanyapaa kwa wagonjwa wanaukutwa
na tatizo hilo.
Alisema
uchunguzi huo umefanyika kwa kipindi cha miaka mitatu kwani saratani ya
mlango wa kizazi ni moja kati ya magonjwa makubwa yanayoua wanawake
wengi katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwakuwa wanawake
wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) wako katika hatari kubwa zaidi ya
kuugua ugonjwa huo.
Taasisi
ya George W. Bush inafadhili mradi wa Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu
(PRRR) ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo uliogharibu zaidi ya dola za
kimarekani milioni mbili ambao pia utazinduliwa hivi karibuni katika
nchi za Namibia na Ethiopia na zikufanya nchi zinazofadhiliwa kufikia
tano.
“Tatizo
kubwa ni Ujinga , upatikanaji wa taarifa zisizo sahihi na unyanyapaa
vinazuia maendeleo ya afya ya jamii na hivyo wanawake kushindwa kwenda
kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi (Human
Papilloma Virus Vaccine) lakini watu wengi wanakufa kutokana na
unyanyapaa ambao uko juu. Naamini unaweza kuvunjwa mara moja kama
kioo”, alisema Mzee Bush.
Aliwahimiza
wake hao wa Marais kuungana kwa pamoja ili kuweza kuimarisha afya ya
mama na wasichana kwani njia moja ya kuwasaidia watoto ni kuwasaidia
mama zao. Na kusisistiza kwamba ni jambo la muhimu kwa watu wanaoishi
na VVU kutokufa kwa magonjwa yanayoweza kutibika na kuzuilika.
Kwa
upande wake Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama alisema wake wa
Marais wa Afrika wana kazi kubwa ya kuzisaidia jamii zao kutokana na
matatizo yanayowakabili kwani wanawake wengi na watoto wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali hasa za afya na elimu.
Kwa
upande wa vijana alisema wanafanya kazi sana katika jamii lakini bado
wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ugonjwa wa Ukimwi. Wao
kama viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa matatizo yao yanatatuliwa.
“Tunaweza
kuwakusanya watu hawa katika meza moja ili kuweza kutatua changamoto
zao, nyie ni sauti za wanyonge wakiwemo wanawake na watoto jitahidini
kuwafikia wanawake wengi zaidi.
Wakati
tunatoa kipaumbele kwa wasichana wetu tunakazi kubwa ya kufanya naamini
majadiliano haya yatatoa jitihada mpya na nini cha kufanya ili tuweze
kuwasaidia vijana wetu, ” alisema Mama Obama.
Mama
Salma Kikwete ni mmoja wa wake wa Marais wa Afrika waliohudhuria
mkutano huo uliandaliwa na Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama
kwa kushirikiana na Taasisi ya George W. Bush ambao ulijadili uwekezaji
katika elimu, upatikanaji wa afya ya wanawake na wasichana na
kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi.
No comments:
Post a Comment