Sunday, August 31, 2014

RAIS KIKWETE APOKEWA NA MABANGO KIBAIGWA MKOANI DODOMA.


Rais Kikwete akisalimiana na wananchi. Picha na Mwandishi Wetu 

Dodoma. Rais Jakaya Kikwete amepokewa kwa mabango na wakazi wa Kibaigwa yaliyokuwa yakielezea kero mbalimbali ikiwamo ukubwa wa ushuru wa mazao.

Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wananchi wakiyainua mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti baada ya Rais Kikwete alipofika kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika juzi ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Dodoma.


Moja ya bango hilo lilikuwa limeandikwa ‘Diwani wa Kibaigwa’ amekuwa chanzo cha kero ya ushuru.


Hata hivyo, baada ya muda mfupi askari polisi waliokuwa wakilinda kwenye mkutano huo, walikwenda na kunyang’anya mabango hayo kutoka kwa waliokuwa wameyabeba.


Akihutubia katika mkutano huo, Rais Kikwete aliahidi kulishughulikia tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji katika mbuga ya hifadhi ijulikanayo kama Emboroy Murtangos kabla ya kumaliza ziara yake mkoani hapa.


“Mwishoni mwa ziara yangu nitakaa na uongozi wa Wilaya ya Kongwa na Wilaya ya Kiteto na uongozi wa Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Dodoma kuona namna gani tusiwe na misuguano kama hii,” alisema.


Alisema aliudhika sana baada ya mmoja wa wakuu wa wilaya kumweleza kuwa hao wakulima wanaoendesha shughuli zao za kilimo katika Wilaya ya Kiteto ni ‘wakuja’.


“Hivi unawasema hawa ni ‘wakuja’ hivi kote mlikoenea nchini mkirudi wote mtaenea? Kwa hiyo wenzenu wakija kulima ni watu wakuja lakini nyie mkienda Kilosa Tanzania ni nchi yetu sote,” alisema na kuongeza kuwa:


“Haiwezekani kuwa changu ni changu, halafu chako ni chetu nchi watu hawaishi hivyo.” Akijibu kero ya ushuru, Rais Kikwete alisema ni jambo ambalo wakazi wa Kibaigwa wanaweza kulishughulikia.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene alisema mgogoro wa Kiteto hausababishwi na matatizo ya ardhi bali ni uongozi na uhusiano.


Awali Mbunge wa Kongwa, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai alisema kwa miaka zaidi 50 wakulima na wafugaji wamekuwa wakiishi kama ndugu lakini jirani zao wamekuwa na sera ya ubaguzi.


Ndugai alisema kwa wakulima wamekuwa wakichomewa mashamba, matrekta, pikipiki. Pia wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano.Alisema maeneo yenye mgogoro ni makubwa na kinachotakiwa ni kuweka mipaka kati ya wakulima na fugaji tu, “Mheshimiwa Rais ni masononeko yasiyokuwa na maelezo, nimechoka kushiriki kwenye mazishi kila leo yanayotokana na kuuwawa kwa

No comments:

Post a Comment