Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema sababu kubwa ya yeye kurudiana na mpenzi wake waliyegombana, Nuhu Mziwanda ni kuombwa msamaha.
Shilole alisema mpenzi wake huyo aligundua kwamba aliteswa na wivu na 
kusababisha wagombane hivyo alipotambua kosa lake, aliomba msamaha 
wakarudiana na mambo yakawa swari.
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana,
 nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema 
Shilole.Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila 
mtu kuchukua hamsini zake.


No comments:
Post a Comment